Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vibe la Wiki: Ghafla tu, mshamuona Aussems ni shida!

Muktasari:

Hivi kweli mashabiki walikwenda uwanjani kusubiri Sevilla wafungwe na Simba? Ama mnadhani kikosi cha Sevilla kilichoanza kilikuwa na dhamira ya dhati kabisa ya kufungwa Afrika tena na Simba?

HAKUNA kitu kizuri katika maisha kama kuweka historia. Ndio! Kwani nani hapendi kuweka historia tena zile tamu tamu si unajua tena. Sasa juzi tu hapo Simba imeweka rekodi ya kukipiga na wababe wa zamani wa Kombe la Ulaya, Sevilla.
Sevilla ambayo inashiriki Ligi Kuu ya Hispania, La Liga, sio Chama la mchezo mchezo hata kidogo na msimu huu imemaliza ikiwa nafasi ya sita. Kwa maana hiyo msimu ujao itakuwa ikishiriki Kombe la Europa na kuwaacha akina Barcelona, Real Madrid kupambana kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Sasa baada ya mashabiki kuzoea kuwaona akina Ever Banega, Jesus Navas na Nolito kwenye luninga tu, juzi wakapata nafasi ya kuwaona laivu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Wachezaji wa Simba nao ni binadamu jamani na wanapenda kutengeneza historia za maisha yao kama walivyo wengine, wenyewe wakapata mzuka zaidi kwa kucheza na masupastaa hao wa Ulaya.
Si ulimuona John Bocco akiweka historia ya kumtungua kipa wa Sevilla, Juan Soriano baada ya kupachika bao la kwanza na kuwainua mashabiki kwenye viti.
Kwa Bocco nadhani baada ya mchezo huo atakuwa amelala akiotoa ndoto nyingi nyingi tu kuhusu Ulaya. Baada ya hapo mvua ya mabao ikafunguliwa bana na mwisho wa mchezo ni kwamba, mabao tisa yaliyokuwa yametikisa nyavu ndani ya dakika 90.
Kati ya mabao tisa hayo, kama kawaida kama dawa Simba anapochomoza kwenye anga za kimataifa huwa na bahati sana ya kukutana na hamsa a.k.a mkono a.k.a Tano.
Lakini, kweye mtanange huo hadi dakika 70 za mwazo ilionekana kabisa kwamba, Simba anakwenda kuandika historia mpya ya kumfunga mbabe wa Ulaya. Mashabiki kwenye majukwaa wakapagawa huku wachezaji wakipandwa mzuka kila wanaposhika mpira hutimua mbio kuelekea alipo Soriano.
Wachezaji na mashabiki na hata baadhi ya vibosile wa Simba, wakasahau kabisa kuwa wanacheza na Sevilla, wakawa kwenye ndoto kama vile wanacheza na Mwadui FC ya kule Shinyanga.
Hata hivyo, kwenye akili ya Mbelgiji, Patrick Aussems, alifahamu kabisa nini kitafuata baada ya kuwa anaongoza kwa mabao 4-2. Alifahamu uwezo na mbinu za kupambana na wachezaji wa Sevilla hana kabisa. Yaani wachezaji wa Simba na Sevilla ni sayari mbili tofauti.
Hapo Aussems akaona isiwe shida akaamua kuwapa vijana wake nafasi ya kuandika rekodi ya kucheza na mastaa wakubwa wa Ulaya kama kina Navas, Banega na Nolito.  Akawaamsha akina Salamba kwenye viti na kwenda kujaribu kuonyesha ubora wao uwanjani. Ndio! Aussems alifahamu mambo yatabadilika muda wowote hivyo, hakuwa na sababu ya kuumiza kichwa.
Jambo la kushangaza ni kwamba, baada ya mchezo eti mashabiki wakaanza kulalamika Aussems amewazingua kwa sub zake kwani, angekiacha kikosi kilichoanza basi wangeshinda mchezo huo.
Akili za mashabiki wa Simba zilishakuwa kwenye kwenda kuwatambia Yanga kwamba, wamemfunga mbabe wa Europa. Jamani soka halina miujiza kabisa. Hivi kweli watu walikwenda uwanjani kwenda kuwashughudia Sevilla wakifungwa na Simba?
Ama mnadhani kikosi cha Sevilla kilichoanza kilikuwa na dhamira ya dhati kabisa ya kufungwa Afrika tena na Simba! Vipi kama wangeanzisha mziki ule ambao ulimsimamisha Jose Mourinho na Manchester United yake pale Old Trafford kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. Mashabiki wa soka wa Bongo wanachotakiwa kushukuru ni kupata nafasi ya kuwaona mastaa hawa ambao wamekuwa wakiwaona kupitia luninga na sio kutarajia miujiuza ya Simba kuifunga Sevilla. Kinachoonekana ni kama mashabiki wa Simba walikwenda uwanjani na matokeo yao mfukoni na mambo yalipokuwa tofauti wakaamua kugeuza kibao kwa Aussems kwamba, alifanya makosa kwenye upangaji wa kikosi. Kwa wanaofahamu misingi ya soka, nadhani watakuwa wamejifunza jambo kwenye ujio wa Sevilla na hata wanavyocheza uwanjani. Tusipende kuwabebesha lawama makocha wakati uwezo wetu unafahamika.