Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vibali vyamtibulia straika mpya Yanga Princess

Vibali Pict

Muktasari:

  • Wachezaji hao ni Mukandayisenga Jeannine kutokea Rayon Sports ya Rwanda na Juliet Nalukenge wa Uganda.

YANGA Princess dirisha hili dogo limesajili washambuliaji wawili wa kimataifa, hata hivyo, wanakabiliwa na changamoto ya vibali (ITC).

Wachezaji hao ni Mukandayisenga Jeannine kutokea Rayon Sports ya Rwanda na Juliet Nalukenge wa Uganda.

Kiongozi mmoja wa Yanga (hakutaka jina lake litajwe) alisema hadi sasa hawajatambulisha wachezaji hao kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo vibali.

Aliongeza, Jeannine hajakamilisha ITC yake na taratibu nyingine za kimakubaliano na klabu yake ya Rayon ambayo bado alikuwa na mkataba wa miezi sita.

"Yupo na timu na anafanya nayo mazoezi, kuna vitu havijakamilika ndiyo maana hajatambulishwa lakini naamini hadi ligi itakapoanza mambo yatakuwa fresh," alisema kiongozi huyo.

Kuhusu Nalukenge alisema "Tulishindwa kuelewena kwenye baadhi ya vitu alikuwa tayari yupo nchini na alianza mazoezi na timu lakini kaondoka ghafla."

Hadi sasa Yanga imetambulisha wachezaji watatu wa ndani, kipa Zubeda Mgunda, kiungo Protasia Mbunda na Diana Mnally.