Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uyole Worriors ndio wababe Mbeya Super Cup

Muktasari:

Mashindano hayo yamedumu kwa siku saba, ambapo jumla ya timu nane kutoka Halmashauri saba za Mkoa wa Mbeya zilishiriki na Uyole Worriors kutwaa ubingwa.

Mbeya. Uyole Worriors wameibuka bingwa wa mashindano ya Mbeya Super Cup baada ya kuigaragaza Kyela Combine bao 1-0 na kujinyakulia kiticha cha Sh 5 milioni.

Katika mchezo huo ambao umepigwa uwanja wa Sokoine jijini hapa timu zote zilionesha ushindani na kandanda safi na kusababisha dakika 45 za awali zinamalizika kwa nguvu sawa ya bila kufungana.

Uyole Worriors ilijipatia bao la ushindi dakika ya 52 lililofungwa na Oscar Adam na kudumu hadi dakika 90 na kuihakikishia timu yake ubingwa na kuandika rekodi ya kuwa timu ya kwanza kuchukua taji hilo kwa msimu wa kwanza wa michuano hiyo.

Kwa matokeo hayo, Uyole Worriors iliondoka na Sh 5 milioni na kombe, Kyela Combine wakabeba Sh 3 milioni na Mbeya DC wakaibuka na Sh 2 milioni kwa kushika nafasi ya tatu baada ya kuwalaza Chunya mabao 3-1.

Akifunga mashindano hayo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesema michuano hiyo itakuwa endelevu na kwamba kwa mwakani wataanzia ngazi ya Kata, Tarafa hadi wilayani.

Amesema kuwa baada ya mashindano hayo, wanaenda kujiandaa tena kuanzisha mengine ambayo yatashirikisha timu kutoka Iringa kama Lipuli na Njombe Mji ya mkoani Njombe sambamba na timu za Mkoa wa Mbeya.

"Haya mashindano yatakuwa endelevu na baada ya kumalizika Mbeya Super Cup tutakuwa na michuano mingine ambayo naikabidhi Chama cha Soka Mkoa, lakini pia mwakani tutashirikisha timu nyingi tukianzia ngazi za Kata na Tarafa" amesema Homera.