Uwanja wa Taifa watikisa Afrika

Dar es Salaam. Katika moja ya mambo yanayochangia kupiga hatua katika soka la Afrika ni ujenzi wa viwanja vikubwa.

Kuanzia 2000 kuna viwanja vingi vimejengwa vimetumia mamilioni ya dola katika ujenzi wake hadi kukamilika kwake hivi hapa ni viwanja kumi ghali Afrika zaidi.

10: Uwanja wa Taifa Dar es Salaam (Dola 53 milioni)

Uwanja huo ulifunguliwa 2007 jijini Dar es Salaam, Tanzania ukipewa na uwezo wa kuchukua mashabiki 60,000, uwanja huo unatumika zaidi kwa mchezo wa soka ukichukua nafasi ya Uwanja wa Uhuru. Uwanja huo ulijengwa kwa kushirikiano na Serikali ya China iliyotoa nusu ya fedha hizo.

9: Uwanja wa Olympique de Rades (Dola 110 milioni)

Uwanja huo una uwezo wa kuingiza watu 60,000 upo mjini Rades, Tunisia. Uwanja huo ulijengwa 2001, kwa ajili ya michezo ya Mediterranea, unasifika kwa kuwa na madhari mazuri.

8: Uwanja wa Mbombela (Dola 140 milioni)

Moja ya viwanja sita vya kwanza vilivyoorodheshwa kwa ajili ya Kombe la Dunia 2010, Afrika Kusini. Kina uwezo wa kuchukua mashabiki 40,929 ndiyo uwanja mdogo zaidi uliotumika kwa Kombe la Dunia. Uwanja huo ulijengwa kwa kodi za wananchi.

7: Uwanja wa Peter Mokaba (Dola 150 milioni)

Uwanja huo upo Polokwame, Afrika Kusini ulitumika kwa Kombe la Dunia pamoja klabu ya Black Leopards FC. Uwanja huo unauwezo wa kuchukua mashabiki 41,733. Uliopewa jina la kiongozi wa zamani wa vijana wa ANC, Peter Mokaba.

6: Uwanja wa 11 de Novembro (Dola 227 milioni)

Ulipewa jina hilo ikiwa ni kumbukumbu ya siku ya uhuru wa Angola. Uwanja wa 11 de Novembro upo mjini Luanda, ulitumika katika michezo ya Mataifa ya Afrika 2010 una uwezo wa kuchukua mashabiki 50,000.

5: Uwanja wa Nelson Mandela Bay (Dola 270 milioni)

Uwanja huo umepakana na ziwa North End mjini Port Elizabeth una uwezo wa kuchukua mashabiki 48,459. Uwanja huo ulipewa jina rais wa kwanza Mzalendo. Ujenzi wake ulikadiliwa kuwa rand 711milioni, lakini ilizidi na kufikia Randi 2 bilioni.

4: Uwanja wa Abuja (Dola 360 nilioni)

Uwanja huo ulijengwa kwa ajili ya Michezo ya Afrika yaliyofanyika 2003 mjini Abuja una uwezo wa kuingiza mashabiki 60,491 ukiwa na kijiji cha michezo. Kwa sasa unatumika kwa mechi za timu ya taifa ya Nigeria.

3. Uwanja wa FNB au Soccer City (Dola 440 milioni)

Uwanja wa First National Bank nchini Afrika Kusini unajulikana zaidi kama Soccer City una uwezo wa kuchukua mashabiki 94,736, baada ya Kombe la Dunia kwa sasa unatumiwa na Kaizer Chiefs.

2: Uwanja wa Moses Mabhida (Dola 450 milioni)

Uwanja huo wa mjini Durban ulitumika kwa Kombe la Dunia 2010 ulikuwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 62,760, lakini sasa wamepunguzwa na kuingia watu 54,000. Kiwanja hicho kimewekea miundombinu ya kisasa zaidi.

1: Uwanja wa Cape Town (Dola 600 milioni)

Uwanja huo zamani ulikuwa ukiitwaa Green Point, una uwezo wa kuchukua mashabiki 64,100 na ulijengwa na kampuni ya Afrika Kusini ya Murray & Roberts.