Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uwanja wa Mkapa bado siku tano

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro amekagua maendeleo ya ukarabati ya awamu ya kwanza yanayoendelea katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar na kusema umefikia asilimia 95 na asilimia tano zilizobaki zinatarajiwa kukamilika ndani ya siku tano kuanzia leo Oktoba 9.

Dk Ndumbaro amesema tayari vyumba vinne vya wachezaji, sehemu ya kuchezea, vyumba vya waamuzi, afya na eneo la video za marejeo (VAR) vimekamilika.

"Tayari taa za kisasa 320 za mfumo wa LED zimefungwa na kuna huduma ya mtandao wa bure kabisa kwa ajili ya watazamaji wa mechi ambao tutauzindua kati ya Oktoba 17 hadi 19 mwezi huu kabla ya mchezo wa ufunguzi wa African Football League kati ya Simba na Al Alhy Oktoba 20, 2023 " amesema Dk Ndumbaro

Ameongeza kuwa, katika eneo la watu mashuhuri (VIP) na sehemu ya wandishi wa Habari kazi iliyobakia ni ndogo ambayo itamalizika ndani ya siku hizo tano akiongeza kuwa mfumo wa sauti uwanjani tayari umerekebishwa.

Dk Ndumbaro amesema kuwa Kampuni ya Formula 360, itafunga mfumo wa matangazo kidijitali ambao utaanza kufanya kazi rasmi Oktoba 20 huku akisistiza kuwa baada ya mchezo huo, ukarabati mkubwa wa awamu ya pili utaendelea.