Usipolipa ada Yanga imekula kwako

Thursday April 08 2021
yanga ada pc
By Thobias Sebastian

UONGOZI wa Yanga, umewataka wanachama wa klabu hiyo kukamilisha haraka malipo ya ada kwa ajili ya maandalizi ya mkutano mkuu, kwani mwanachama atakayeshindwa kufanya hivyo atakosa fursa ya kuhudhuria mkutano huo utakaofanyika mwezi ujao.


Katika taarifa iliyotolewa na klabu hiyo leo Aprili 8, imewataka wanachama wenye aina zote za kadi za uanachama zinazotambuliwa na klabu kulipa ada ya mwaka mmoja huku ikielekeza namna ya malipo hayo yanavyopaswa kulipwa kwa njia ya benki na mitandao ya simu.


Hata hivyo taarifa hiyo imeleza hayo ni maandalizi kwa ajili ya mkutano mkuu ambao unatarajiwa kufanyika Mei jijini Dar es Salaam.

Taarifa hiyo ilieleza zaidi mwanachama anatakiwa kulipa mapema ili awe na uhalali wa kushiriki mkutano huo muhimu kwa ajili ya maendeleo ya klabu.


Miongoni mwa mambo makubwa ambayo yanatarajiwa kuzungumzwa katika mkutano mkuu ni kuhusu mchakato wa mabadiliko mahala ulipofikia pamoja na masula mengine ya msingi.

Advertisement