Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uongozi Singida United wampongeza Mwigulu, kuwaombea ligi ifutwe

WAZIRI Waziri mpya wa Katiba na Sheria, Mwigullu Nchemba

Muktasari:

Singida United inashika mkia katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ikiwa imekusanya jumla ya pointi 15 katika mechi 29.

WAZIRI Waziri mpya wa Katiba na Sheria, Mwigullu Nchemba akiapishwa leo Jumapili, uongozi wa Singida United umetoa pongezi kwake lakini ukikiri kuwa bado una kazi ya ziada kuhakikisha timu hiyo inabaki Ligi Kuu.
Tofauti na mawazo ya wengi kuwa uteuzi wa Mwigulu unaweza kuwa chachu ya timu hiyo kufanya vizuri na kubaki Ligi Kuu licha ya kushika mkia katika msimamo wa ligi kwa sasa, wenyewe Singida United wamekiri kuwa wana mlima mrefu wa kupanda ili wanusurike.
"Tunampongeza Mheshimiwa Mwigulu kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Ni jambo la kujivunia kuona Rais amekuwa na imani naye na akamteua kushika nafasi hiyo.
"Lakini kusema kuwa Singida United sasa ina uhakika wa kubaki kwa sababu ya uteuzi huo sidhani kama ni sahihi kwa sababu timu ipo katika nafasi mbaya na pia wapinzani wetu nao wana michezo waliyoibakiza ambayo wanaweza kupata ushindi.
"Kikubwa kinachoweza kuinusuru timu ni kufutwa kwa ligi na si vinginevyo, ligi ingefutwa tu ili tujipange upya na msimu ujao " amesema mmoja wa Wakurugenzi wa timu hiyo Yusuph Mwandami.
Kiongozi mwingine wa timu hiyo, Abdulrahman Sima alisema kuwa kuteuliwa kwa Mwigulu hakuifanyi timu yao ijihakikishie kubaki Ligi Kuu
"Uteuzi huu tumeupokea vizuri lakini sio sababu ya timu kufanya vizuri na kubaki kwenye ligi" amesema Sima ambaye ni Katibu Mkuu wa Singida United.
Singida United kwa sasa ipo mkiani mwa msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi zake 15 ilizokusanya baada ya kupata ushindi katika michezo mitatu, kutoka sare mara sita na kufungwa michezo 20.