Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Unataka kuwa Ronaldo? Pita humu mwanangu utatoboa

Muktasari:

  • Katika umri wa miaka 34 alionao, Ronaldo amefanikiwa kutwaa jumla ya mataji 26, akishinda tuzo ya Ballon d'Or mara tano na akichukua Kiatu cha Ufungaji Bora Ulaya mara nne.

TURIN, ITALIA, FEBRUARI 5, Cristiano Ronaldo atagonga miaka 34. Lakini, kwa sasa mwili wake alivyoujenga, amekuwa kama kijana wa miaka 23.
Kutokana na hilo, bila ya shaka atatimiza ndoto zake za kuendelea kucheza soka hadi kwenye umri wa miaka 40.
Akiwa na umri wa miaka 33 kwa sasa, supastaa huyo anayekipiga kwenye kikosi cha Juventus amekuwa moto na haonekani kabisa kukata moto wake kwenye suala la kupasia mipira kwenye nyavu za timu pinzani.
Huko kwenye Serie A tayari ameshafunga mabao 12. Ronaldo mwenyewe anasema mwili wake unamfanya ajione kuwa kijana wa miaka 10 nyuma kutoka kwenye umri wake wa sasa, hivyo anataka kuendelea kutamba kwenye soka hadi atakapofika umri wa miaka 41 huko.
Akiwa na kimo cha fupi 6 na nchi 2, fowadi huyo ameufanya mwili wake kujengeka kimazoezi kwelikweli na kuwa tishio kwa mabeki wa timu pinzani, huku akiendelea kuwa kiboko kwa mipira ya juu.
Mapema mwaka huu, Ronaldo alisema: "Umri wangu wa sasa najiona kama nina miaka 23. Bado nina muda mwingi sana umebaki, nitaendelea kucheza hadi nitakapofika umri wa miaka 41. Najisikia vizuri, nafurahia na silalamiki."
Lakini, ushawahi kujiuliza, hivi Ronaldo anafanya nini na anakula kitu gani kuwa na mwili huo matata kabisa?
Unaambiwa hivi, anachofanya Ronaldo sio siri, ni tizi tu kwa kwenda mbele na kupiga misosi ya uhakika. Kitu kingine, Ronaldo anajipa muda mwingi wa kupumzika na hiyo misusi yake, anakula mlo kamili na wenye uangalizi mkubwa. Kuogelea pia ni sehemu ya mambo anayofanya Ronaldo ili kujiweka fiti muda wote, kuwa na mwili wa kijanja kwenye umri wa kizee.
Kitu kingine ambacho Ronaldo amekuwa akifanya kujiweka fiti ni kufanya mazoezi makali sana kabla ya mechi na amekuwa akifanya hivyo kivyake bila ya kusukumwa na kocha wake.
Wakati wachezaji wengine wakipenda kuketi kwenye televisheni baada ya mechi, Ronaldo yeye anakwenda moja kwa moja kwenye bwawa la kuogelea na kupoza misuli yake moto. Anaogelea kwa muda kwani jambo hilo kumfanya kupoza misuli yake na pia kuijenga zaidi katika kuifanya kuwa yenye ukakamavu zaidi. Kuogelea ni mazoezi ya mwili mzima.
Ronaldo pia anavifaa vyote vya gym nyumbani kwake. Sambamba na vifaa hivyo vya gym, Ronaldo pia ana chumba maalumu cha mazoezi ya mvuke. Ronaldo amekuwa akiingia kwenye chumba hicho na kukaa kwa dakika tatu ambapo mashine iliyomo kwenye chumba hicho inasaidia kuweka sawa na kuondoa maumivu yote mwilini.
Kulala ni kitu kingine ambacho Ronaldo amekuwa akikifanya bila ya kukosa, ambapo amekuwa akitumia saa nane kulala. Ronaldo ana mabafu ya maji moto na maji baridi ili kukuza misuli yake. Kitu kingine anachofanya Ronaldo ni kupumzika.
Kulikuwa na ripoti kwamba Ronaldo amekuwa akifanya mazoezi ya simama kaa mara 3,000 kwa siku, mwenyewe amedai huwa hafanyi sana mazoezi ya aina hiyo, amekuwa akifanya hivyo mara 1,000 kwa wiki. Alisema mazoezi mengi ya aina hiyo ya kusimama na kukaa, yanasababisha majeruhi na kuchosha misuli.
Kuhusu misosi, Ronaldo amekuwa hafanyi mzaha. Ronaldo anapenda sana kula samaki, mayai pamoja na salad. Hagusi vyakula vyenye sukari na nyama za kusindikwa. Utotoni kwake, Ronaldo alikuwa mwembamba sana, lakini mazoezi yamefanya kwa sasa aonekane kuwa na mwili jumba. Ronaldo amefanya hivyo baada ya kusikia mmoja wa makocha wake kuuponda mwili wake goigoi, wakati huo alipokuwa na umri wa miaka 11.
Kocha huyo alimwambia Ronaldo, unamwona mtoto mwenzako yule, yupo fiti na hilo ndilo lililomfanya Ronaldo kufanya mazoezi kuwa na mwili wa kibingwa ndani ya uwanja ili kuwapa shida mabeki wa timu pinzani.
Lakini, mazoezi yote hao ya Ronaldo yasingekuwa na maana kama asingefuata masharti ya mlo wake. Ronaldo hapendi mboga za majani au zile zinazotokana na mimea, lakini anahakikisha kwamba hali nyama nyingi kwa sababu ya kukwepa mafuta. Samaki ndio chakula chake kikuu, vitunguu, viazi na mayai. Ronaldo mwenyewe anasema anapenda kula vyakula vya protini zaidi, matunda na mbogamboga kiasi, lakini akijiweka mbali kabisa na vyakula vyenye sukari. Mama yake Ronaldo, Dolores Aveiro ni mtu muhimu sana katika kuhakikisha mwanaye anapata mlo anaoupenda na kuendana na kazi yake anayofanya.