Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ujanja wote wa Massawe upo hapa buana!

Muktasari:

Ukisikia mapenzi niue basi ni kwa hawa wanandoa, mke wa Massawe anasimulia namna ambavyo mume wake anam thamini, kupenda na kumjali anajiona ni malkia mbele ya mfalme.

UKITAJA wachezaji wenye nidhamu ya hali ya juu nchini, basi jina la Jacob Massawe, nahodha wa Gwambina FC ya Ligi Daraja la Kwanza, haliwezi kukosekana na hilo linatokana na mke mwema anayemsimamia mambo yake.

Beatrice Dindai ni mke halali wa Massawe, aliyefunga naye ndoa mwaka 2012 katika Kanisa la Mama Mwenye Huruma lilipo Shinyanga baada ya kudumu kwenye uhusiano kwa muda wa miaka minane tangu wajuane 2005. Wakiwa kidato cha pili Shule ya Sekondari ya Uhuru, iliopo mjini Shinyanga.

Ukisikia mapenzi niue basi ni kwa hawa wanandoa, mke wa Massawe anasimulia namna ambavyo mume wake anam thamini, kupenda na kumjali anajiona ni malkia mbele ya mfalme.

Anasema Massawe ni mume wa ndoto na miujiza kwake, akisisitiza ni wachache wenye moyo wa kupenda familia na kila kitu chake kuwa sehemu yao.

“Ni mume mwema, ana hofu ya Mungu na anapenda sisi tule vizuri, tuvae vizuri na tuishi sehemu nzuri, tangu nijuane naye sijawahi kujuta, kila wakati naona mpya,” anasema.

Licha ya mwaka 2005 ndipo alipofuata kuambiwa anapendwa na anahitaji awe mke wake, walikutana kwa mara ya kwanza mwaka 2003 wakati anakwenda kuangalia matokea ya darasa la saba katika ofisi za halimashauri za mkoa huo.

“Nilikuwa nasoma Mwenge na yeye alikuwa anasoma Bugoi, aliponiaona akanitazama kwa muda mrefu kisha akauliza jina, nikamwambia akaanza kuniangalizia matokeo, mwisho wa siku tukajikuta wote tumefaulu katika Shule ya Uhuru,” anasema na kuongeza;

“Nilishangaa kuona anafuraha ya ajabu baada ya kuchaguliwa shule moja, nilikuwa simjui wala hanijui, baadaye ndipo akaja akaniambia ndio mwanzo wake wa kunipenda, basi safari ikaendelea mpaka hapa tulipofika.”

NI WAKALA WAKE

Beatrice anasema ni kama wakala wa mume wake kutokana na kila anapopata timu lazima waamue kwa pamoja ndipo akafanye maamuzi ya kusaini au la.

“Hata huko Gwambina FC alikokwenda mimi ndiye niliyemwambia akubali ofa yao, kifupi mimi ni maisha yake na yeye ni maisha yangu ni rafiki yangu namba moja wengine wanafuata,” anasema.

HAPA MASSAWE ALICHEMKA

Anasema siku moja mume wake alimdanganya baada ya yeye kubaini alikwenda disko na kunywa pombe jambo ambalo hakuwahi kuliona kwake, anakiri lilikwaza kiasi cha kumnunia.

“Nilichukia sana, baadaye alipoona imani ya kumwamini inanitoka akanikalisha chini na kuniambia mke wangu nisamehe, nilienda kweli na marafiki zangu disko na nikanywa pombe, nilishindwa kukiri kwa sababu sikutaka nikukwaze.

“Nikajikuta hasira imeisha hadi namuonea huruma, basi tukaendelea kupendana na hilo sikuliona kujirudia, kiukweli nashukuru Mungu kunipa mume ambaye naelewana naye sio wote wana bahati hiyo,” anasema.

WANA MTOTO MMOJA

Anasema wamebahatika kupata mtoto mmoja anayeitwa Catherine (3) na kwamba wana mpango wa kupata wengine kadiri Mungu anavyowajalia.

“Kipindi ambacho nilikaa naye muda mrefu ni hiki ambacho alikuwa na Stand United kabla ya kushuka daraja, ndipo akapatikana binti yetu, ingawa hata akiwa mbali lazima apige simu kujua tumeamkaje, mchala tunaendeleaje na usiku kututakia kheri,” anasema.

MASSAWE AKIWA NA HASIRA

Anasema amemjulia mume wake akiwa na hasira hata akimfokea anakuwa ananyamaza kimya mpaka anapomuona moyo wake umetulia ndipo anakwenda kumuelewesha jambo linalomfanya achukie.

“Hapendi kudanganywa na sipendi kudanganywa, hilo linatufanya tuendelee kudumisha upendo wetu, hata nikikosea naongea ukweli tunakaa chini ananisamehe,” anasema.

ANAFUNGA

Anasema anapata muda wa kumuombea mume wake ili Mungu ambariki na majukumu yake huwa ili asije akajihusisha na imani za kishirikina.

“Mbali na kufunga kila anapoingia kwenye mechi napiga goti naomba, sisi tunamtegemea Mungu najua ni kweli kwenye soka kuna mambo mengi, ila Mungu ni juu ya kila kitu,” anasema.