Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ufudu ajilipua Mashujaa

Muktasari:

  • Ufudu ni usajili wa kwanza kutambulishwa na Mashujaa kwenye dirisha hili akifuatiwa na Yusuph Dunia kutoka Geita Gold, baada ya kuachana na wachezaji wao tisa akiwemo Reliants Lusajo, Adam Adam na Samson Madeleke.

BAADA ya kudumu Kagera Sugar kwa miaka minne, Julai 7, mwaka huu kiungo, Ally Nassoro Iddi ‘Ufudu’ alitua Mashujaa FC ya Kigoma akisaini mkataba wa mwaka mmoja, huku akifichua siri ya kujiunga na maafande hao na yuko tayari kupambania namba kikosini hapo.

Ufudu ni usajili wa kwanza kutambulishwa na Mashujaa kwenye dirisha hili akifuatiwa na Yusuph Dunia kutoka Geita Gold, baada ya kuachana na wachezaji wao tisa akiwemo Reliants Lusajo, Adam Adam na Samson Madeleke.

Wengine walioachwa na Mashujaa ni Mchembe Maganda, Ally Ramadhan (Oviedo), Michael Masinda, Said Makapu, Shadrack Ntabindi na Omary Abdallah aliyetua Simba.

Kiungo huyo alijiunga na Kagera Sugar msimu wa mwaka 2020/2021 akitoka Mbeya City na Julai, 2022 aliongezewa mkataba wa miaka miwili ambao umemalizika Julai, mwaka huu na kusajiliwa Mashujaa FC akiwa mchezaji huru kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Ufudu aliliambia Mwanaspoti masilahi mazuri ndiyo yameng’oa Kagera Sugar huku akitamba yuko tayari kwa ushindani wa namba na kuhakikisha anaisaidia timu yake mpya kufanya vizuri Ligi Kuu.

“Mpira ni kazi yangu niko tayari kufanya kazi na timu yoyote inayokuja kwangu, masilahi ndiyo yanayonivuta kwa hiyo Kagera Sugar nilimaliza mkataba, nimeona masilahi yamenivutia nikaondoka na kuamua kuja Mashujaa,” alisema Ufudu na kuongeza;

“Ligi Kuu ya msimu ujao kutakuwa na ushindani mkubwa na hata kwenye kikosi chetu ushindani utakuwepo, hivyo, nimejiandaa kuhakikisha napata nafasi na kutumikia timu yangu.”