UCHAMBUZI: Simba iwadhibiti Al Ahly maeneo haya

Saturday February 20 2021
New Content Item (1)

 MSIMU wa Ligi ya Mabingwa Afrika uko kwenye harakati zake na wawakilishi wetu Simba wanajindaa na mechi dhidi ya Al Ahly itakayochezwa Jumanne ijayo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dares Salaam.

Simba wapo katika kundi A ambalo mbali na Al Ahly kuna pia timu za AS Vita Club ya DR Congo na El Merreikh ya Sudan.

AS Vita na El Merreikh kama ilivyo kwa Al Ahly ni timu kubwa na ngumu zenye historia kubwa ya soka Afrika zikiwa zimewahi kufanya vizuri hapo nyuma.

Tukija katika mchezo ambao Simba watacheza na Al Ahly, wawakilishi wetu hapana shaka watakuwa na mchezo mgumu na wanapaswa kufanya kazi ya ziada kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo.

Kuna sifa za nje na ndani ya uwwnja ambazo Al Ahly wanazo zinazofanya mechi yao dhidi ya Simba hapa iwe ya aina yake.

Kwanza nje ya kiwanja, Al Ahly ni timu kubwa. Unaposema next level wao wako huko kwa maana kwamba wana uwekezaji mkubwa na wako imara kiuchumi. Lakini la pili ni mabingwa watetezi.

Advertisement

Walichukua 2021 taji hilo msimu uliopita hivyo kote waliko wanatembea na sifa hiyo. Pia wametoka katika kombe la dunia la klabu.

Wakati sisi kucheza makundi tunashangilia wenzetu wanacheza dunia kwa hiyo unaweza kuona gap hapoTunaposema next level lazima tujitathmini kwamba je kile ambacho wenzetu wanacho sie tunacho?

Wana benchi jipya ambalo liko chini ya kocha Pitso Mosimane. Uwepo wake unategemewa kufanya kitu kikubwa.

Timu kama bingwa wanapoleta mwalimu mpya maana yake wanataka kuendelea kwa kile wanachokifanya

Sifa nyingine ya nje ya kiwanja wenzetu wamekuwa wakienda back to back katika hatua ya makundi na sio mara moja wamekuwa wakienda mara nyingi.

Uzoefu wao ni mkubwa na wa ngazi za juu. Ndio maana lazima tuite ni timu kubwa kutokana na historia yakeWana squad pana. Wote ni potential na wana wachezaji bora. Mchezaji mmoja anasajiliwa kwa fedha wanayosajiliwa wachezaji karibia wote wa Simba hivyo wachezaji wote ni lazima wawe na timu bora.


 Ni lazima tujue ubora na sifa za watu ambao timu zetu zinakwenda kucheza nao. Waweze kujiandaa kwa heshimaKiwanjani yako mambo mengi ambayo nimeyaona kupitia ligi ya mabingwa Afrika na Kombe la Dunia la klabu ambalo wametoka kucheza na wakamaliza wakiwa nafasi ya tatu.

Wachezaji wao wengi ni skillful players. Wana mbinumbinu za kuonyesha uwezo wao dhidi ya wapinzani. Ni timu ambayo inacheza kwa kasi sana hasa kwenye flanks. Wachezaji wao wa pembeni Wanakimbia sana na kupiga krosi langoni mwa mpinzani.Wana fighting spirit kwa dakika 90.

Mfano mchezo wa juzi dhidi ya El Merreikh kipindi cha kwanza walionekana hawajaweza kupata ushindi lakini kipindi cha pili wakaweza kufunga mabao matatu.Wana tabia ya kuslow down mchezo kwa maslahi yao ili kupunguza presha ya wapinzani. Ambao ofcourse kimbinu inakubalika ila hawa wenzetu wanajua ni kwa wakati gani wa kufanya hivyo.

Simba wasiingie katika huo mtego. Wanaonekana ni wazuri wa kusoma mchezo. Game reading and understanding. Inawasaidia kwenda sambamba na mchezo na hii inategemea na uwezo wa mchezaji mmojamoja au idara nzima.

Wana footwork nzuri lakini pia wako bora katika aerial management. Wana maumbo mazuri. Unapiga mpira wa juu hauwasumbui na ground movements.

Pia ni wazuri katika set pieces. Wanalazimisha fouls. Pia ni wazuri katika group play. Wote wanashiriki katika kushambulia na kuzuia.

 Wanashiriki vyema katika phase hizo mbili za mechi.Ni wazuri wa mashambulizi ya kushtukiza hasa mabeki wa pembeni. Quick restart. Tunasema fast break.

 Wana beki ambayo iko connected. Ambayo haiwezi kuvunjika vunjikaLakini pia wana wachezaji ambao wanakimbia sana hasa kwenye final third.

Pia wako well organized katika midfieldWanatumia 4-3-3, 4-2-3-1 ama 3-5-2 wanabadilika kulingana na opponent wao. Hasa kipindi cha pili. Game ya bayern Wana high concentration hasa katika eneo la mwisho.

Umakini wao unaongezeka kadri wanavyolisogelea goli. Wanajaribu kutumia nafasi chache wanazopata.Wana mawasiliano mazuri.

Kipa anaongea na walinzi wake nao wanaongea na viungo wao ambao nao wanawasiliana na wa mbele. Visual communications.

Wana mapungufu yao wana kitu kinaitwa mind game kwa mwamuzi. Mara wanapokuwa wamepata goli wana tabia ya kujiangusha kumhadaa refa

Wanapokuwa under pressure kama mmewabana vizuri wanapoteza mawasiliano hasa kwenye backline.

Wakiwahi kufungwa hasa goli la mapema wanahamaki. Wako emotional kidogo. Ni faida kwa timu pinzani kuwawahi na kutumia udhaifu huo. Simba wacheze kwa kujitolea. Wana advantage wanacheza nyumbani.

 Huko nje hakuna mashabiki. Watumie fursa hiyo ili kuishinda mechi ya awali, wanapokwenda ugenini watakuwa wakiwa vizuri. Wacheze dakika 90.

Advertisement