Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

UCHAMBUZI: Kwanini usajili wa Mwenda Yanga?

Mwenda Pict

Muktasari:

  • Hayo ni maswali wanaojiuliza wapenzi na mashabiki wa Yanga baada ya jana asubuhi, uongozi wa Yanga kumtambulisha beki huyo wa kulia anayemudu pia kucheza kushoto na eneo la winga zote ambaye fasta aliibukia mazoezini smbamba na wachezaji wa kikosi cha sasa cha Kocha Sead Ramovic.

KWA nini Yanga imemsajili Israel Patrick Mwenda? Wameona nini kwake? Usajili wake una maanisha nini na je ataweza kupindua meza baada ya kushindwa mbele ya Shomari Kapombe wakati alipokuwa Simba?

Hayo ni maswali wanaojiuliza wapenzi na mashabiki wa Yanga baada ya jana asubuhi, uongozi wa Yanga kumtambulisha beki huyo wa kulia anayemudu pia kucheza kushoto na eneo la winga zote ambaye fasta aliibukia mazoezini smbamba na wachezaji wa kikosi cha sasa cha Kocha Sead Ramovic.

Wanayanga wamekuwa na mitazamo tofauti juu ya usajili huo, wakiona kama hawezi kuwa na maajabu mbele ya Yao Kouassi na Chadrack Boka wanatumika beki za pembeni.

Sio Boka na Yao, lakini Mwenda anaenda kuungana na Kibwana Shomary na Nickson Kibabage ambao ni wazi mmojawao ni lazima watampisha beki huyo wa zamani wa Simba na Singida BS.

Mijadala imekuwa mikubwa juu ya utambulisho wa Mwenda, lakini Mwanaspoti katika fukunyua yake imenasa taarifa za kwanini mabosi wa klabu hiyo wameamua kumnasa beki huyo wa zamani wa Alliance FC.

Mashabiki wanajiuliza mtandaoni, Yanga imeona nini kwa beki huyo na je atapindua meza baada ya kuchemsha kwa Shomary Kapombe alipokuwa Msimbazi kiasi cha wawili hao kuchuniana na kuugawa uongozi wa klabu hiyo ya nani aondoka na nani abaki katika dirisha lililopita kabla ya kuibukia Singida BS.

Taarifa hizo zinabainisha kwamba, Mwenda alikuwa kwenye hesabu za Yanga Yanga tangu usajili wa dirisha kubwa msimu huu, lakini dili hilo likafa kutokana na kuwa na mkataba na Simba na iliposikia ameibukia Singida waliona ni nafasi rahisi kwao kumbeba na ndivyo kilichotokea na kutambulishwa rasmi jana.

Sababu ya Yanga kumtaka beki huyo ni uwezo wa kucheza beki ya kulia na kushoto na hata eneo la wingi ndio maana ilikuwa ikimpigia hesabu kwa muda mrefu.

Uhusiano mzuri wa klabu hizo mbili za Yanga na Singida imetajwa ni sababu ya Mwenda kutua Jangwani kirahisi, kwani hapo awali zilishabadilishana wachezaji katika kipindi cha usajili wa dirisha kubwa msimu huu ambapo Joseph Guede na Metacha Mnata walitoka Yanga kwenda Singida, huku Yanga ikimsajili Khomeini Abubakar kutoka Singida iliyokuwa ikifahamika kama Ihefu.


NAFASI YAKE

Usajili wa Mwenda unakuwa ni wa kwanza chini ya Kocha Ramovic aliyetambulishwa Novemba 15 mwaka huu akichukua nafasi ya Miguel Gamondi.

Mwenda kutua kwake Yanga inamaanisha sasa timu hiyo itakuwa imepata beki kiraka anayemudu kucheza beki wa kulia na kushoto, lakini pia mwenye uwezo wa kucheza winga na kumrahisishia kazi Ramovic kumchezesha katika mfumo wa 3-5-2 unaotumia zaidi mabeki watatu nyuma.

Katika mfumo wa 3-5-2, mabeki wa pembeni (wing-backs) wana jukumu muhimu na la kipekee. Mfumo huu unajumuisha mabeki watatu (center-backs) na wachezaji watano katikati ya uwanja ambapo mabeki wa pembeni wanakuwa sehemu muhimu ya kuunganisha ulinzi na mashambulizi.

Kwa kifupi, mabeki wa pembeni katika mfumo wa 3-5-2 wanachukua majukumu ya kuungana na timu ya ulinzi na mashambulizi kwa nyakati tofauti. Wakati timu inashambulia wanapaswa kwenda kuongeza nguvu, lakini mashambulizi yakirudi kwao hawana budi kurudi kwa wakati kukaa kwenye maeneo yao kuzuia hatari.


VITA IPO HAPA

Ujio wa Mwenda utamuweka katika wakati mgumu beki wa kulia, Kibwana Shomari aliyeonekana kushindwa kupenya mbele ya Yao, lakini hata kwa Kibabage anayecheza beki ya kushoto naye atakuwa na kazi kubwa ya kufanya ili kusalia kikiosini kwani bado amekuwa akiwekwa benchi na Boka aliyesajiliwa dirisha kubwa.


AANZA MAZOEZI

Taarifa kutoka Yanga zimefichua kwamba, saa chache baada ya kumtambulisha Mwenda kikosini hapo, haraka alianza mazoezi na wenzake yaliyofanyika jana Jumatano asubuhi kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam.

Yanga inajiandaa na mchezo wa tatu wa Kundi A katika Ligi ya Mabingwa Afrika ugenini dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo utakaochezwa Jumamosi ya wiki hii nchini humo.

Hayo ni miongoni mwa maswali ambayo mashabiki wa Yanga na soka kwa ujumla wanajiuliza hivi sasa.

Maswali hayo yanaibuka ikiwa ni saa chache baada ya Yanga kumtambulisha Israel Mwenda kuwa mchezaji wao wakimchukua kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu kutokea Singida Black Stars.

Taarifa zinabainisha kwamba, Mwenda alihitajika na Yanga tangu usajili wa dirisha kubwa msimu huu, lakini dili hilo likafa kutokana na kuwa bado na mkataba na Simba.

Hata hivyo, Yanga haikukata tamaa kwani iliendelea kumfuatilia nyota huyo mwenye uwezo wa kucheza beki wa kulia na kushoto ili kuona itawezaje kumpata kirahisi hata mbele ya safari kwani bado ilikuwa na malengo naye.

Baada ya Mwenda kutua Singida Black Stars iliyokuwa ikinolewa na Patrick Aussems, Yanga ikaona huu ndio wakati sahihi kwao kumsajili kutokana na kwamba timu hizo zimekuwa zikifanya biashara nzuri ya wachezaji bila ya kuwekeana ngumu.

Mahusiano mazuri ya timu hizo yamefanikisha madili kadhaa ya wachezaji katika kipindi cha usajili wa dirisha kubwa msimu huu ambapo Joseph Guede na Metacha Mnata walitoka Yanga kwenda Singida Black Stars, huku Yanga ikimsajili Khomeini Abubakar kutoka Singida Black Stars ambayo zamani ilifahamika kwa jina la Ihefu.

"Endapo Mwenda atafanikiwa kufanya vizuri huenda Yanga ikafanya biashara ya kumnunua moja kwa moja beki huyo kutokana na uwepo wa kipengele hicho kwenye mkataba wake wa mkopo," alisema mtu wa karibu na beki huyo.


NAFASI YAKE YANGA

Usajili huo wa Mwenda kwenda Yanga ni wa kwanza chini ya Kocha Mkuu, Sead Ramovic aliyetambulishwa kikosini hapo Novemba 15 mwaka huu akichukua nafasi ya Miguel Gamondi.

Mwenda kutua kwake Yanga inamaanisha sasa timu hiyo itakuwa imepata beki kiraka anayemudu kucheza beki wa kulia na kushoto, lakini pia mwenye uwezo wa kucheza winga na kumrahisishia Kocha Ramovic kumchezesha katika mfumo wa 3-5-2 unaotumia zaidi mabeki watatu nyuma.

Katika mfumo wa 3-5-2, mabeki wa pembeni (wing-backs) wana jukumu muhimu na la kipekee. Mfumo huu unajumuisha mabeki watatu (center-backs) na wachezaji watano katikati ya uwanja ambapo mabeki wa pembeni wanakuwa sehemu muhimu ya kuunganisha ulinzi na mashambulizi.

Kwa kifupi, mabeki wa pembeni katika mfumo wa 3-5-2 wanachukua majukumu ya kuungana na timu ya ulinzi na mashambulizi kwa nyakati tofauti. Wakati timu inashambulia wanapaswa kwenda kuongeza nguvu, lakini mashambulizi yakirudi kwao hawana budi kurudi kwa wakati kukaa kwenye maeneo yao kuzuia hatari.


VITA ITAKUWA HAPA

Ujio wa Mwenda katika kikosi cha Yanga utamuweka kwenye wakati mgumu beki wa kulia, Kibwana Shomari ambaye ameonekana kushindwa kumpa changamoto Yao Kouassi. Lakini pia  Nickson Kibabage anayecheza beki ya kushoto naye atakuwa na kazi ya kufanya kutokana na Mwenda kuwa na uwezo wa kucheza nafasi hiyo ambayo Chadrack Boka ndiye chaguo la kwanza.


ILIKUWAJE SINGIDA BLACK STARS?

Mwenda ndani ya Singida Black Stars, hakuwa na wakati mzuri kwani nafasi ya beki wa kulia alikutana na changamoto ya namba mbele ya Ande Koffi Cirille raia wa Ivory Coast.

Lakini pia upande wa kushoto ambapo Mwenda anaweza kucheza, kuna Ibrahim Imoro, hivyo kuifanya nafasi yake kuwa finyu chini ya Kocha Patrick Aussems ambaye aliondolewa Novemba 29, mwaka huu.


SIMBA JE?

Mwenda alikwama kudumu ndani ya Simba kufuatia uwepo wa Shomari Kapombe ambaye ndiye alikuwa chaguo la kwanza kwa kipindi cha misimu mitatu aliyocheza kikosini hapo akitokea KMC.

Licha ya kwamba hakuwa akipata nafasi ya kucheza mara kwa mara, lakini kila alipopewa nafasi alionyesha uwezo mkubwa ambao leo hii umewafanya Yanga kumsajili nyota huyo aliyewahi kuitumikia Allince ya Mwanza iliyomtambulisha katika Ligi Kuu Bara msimu wa 2018/19.

Mwenda mwenye miaka 24, alikuwa miongoni mwa wachezaji waliounda kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 'Serengeti Boys' kilichoshiriki Fainali za Mataifa Afrika kwa vijana kwa umri huo mwaka 2017 nchini Gabon.

Beki huyo alikuwa timu moja na nyoya wanaocheza Yanga hivi sasa Kibwana Shomari, Nickson Kibabage na nahodha wao msaidizi Dickson Job.