Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uchaguzi Yanga wazidi kunoga

Muktasari:

  • UCchaguzi wa mwisho wa Yanga ulifanyika Mei 5, 2019 na Dk Mshindo Msolla aliibuka kidedea kwa kuchaguliwa kwa jumla ya kura1276 dhidi ya 60 alizopata Dk Jonas Tiboroha, huku Fredrick Mwakalebela akishinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti kwa kura 1206

MBIO za Uchaguzi Mkuu wa Yanga wa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi wa klabu hiyo kongwe nchini, umezidi kunoga kwa wagombea waliojitokeza kuchukua fomu watakaporudisha mchana huu.
Uchaguzi wa Yanga unatarajiwa kufanyika Julai 10, jijini Dar es Salaam ili kuchukua nafasi za viongozi wa sasa wanaomaliza muda wao chini ya Mwenyekiti, Dk Mshindo Msolla na Makamu wake, Fredrick Mwakalebela.
Taarifa kutoka ndani ya Kamati ya Uchaguzi huo wa Yanga inayoongozwa na Ally Mchungahela  zinasema wagombea waliochukua fomu wataanza kuzirudisha leo ikiwa ndio siku ya mwisho ya mchakato wa kuchukua na kurudisha fomu hizo.
Nafasi kubwa zinazosubiriwa kujulikana nani amechukua fomu ni kwa wagombea wa nafasi za Urais na Makamu wake ambapo kiu ya wengi wanasubiri kujua majina kamili ya vigogo wanaowania nafasi hizo.
Nafasi nyingine inayowaniwa kwenye uchaguzi huo ni Ujumbe wa Kamati ya Utendaji na uchaguzi huo ni wa kwanza kwa Yanga tangu klabu hiyo ilipopitisha mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji ikitoka kuwa chini ya wanachama hadi kuendeshwa kama kampuni.