Uchaguzi Simba wapigwa teke

Muktasari:

Mchezo wa JKT Tanzania umesababisha mabadiliko ya tarehe uchaguzi kwa viongozi wa Simba lengo likiwa ni kuwapa fursa mashabiki wa timu hiyo kwenda kuiongezea nguvu timu yao na sasa unatarajia kufanyika Novemba 4.

KAMATI ya Uchaguzi ya Simba imesogeza mbele uchaguzi wao uliopangwa kufanyika Novemba 3 na sasa utafanyika Novemba 4 ikiwa ni mabadiliko ya siku moja pekee.

Mabadiliko ya uchaguzi huo ni kutokana na muingiliano wa mechi ya Simba na JKT Tanzania itakayochezwa Novemba 3 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, mabadiliko hayo yameingiliana na siku ya Mkutano Mkuu wa Simba ambao umepangwa kufanyika Novemba 4.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Boniface Lyamwike, aliliambia Mwanaspoti kuwa muingiliano wa Mkutano Mkuu na Uchaguzi mkuu hautaathiri jambo lolote kwani wanachama wanaohusika ni hao hao.

“Hatuwezi kuwachanganya wanachama wetu kuwafungia kwa ajili ya uchaguzi wakati timu yao itakuwa uwanjani ikiumana na JKT Tanzania tumeamua kusogeza mbele uchaguzi kwa lengo la kuwapa nafasi mashabiki wetu ili waende kuongeza nguvu.