Tulia kuwashuhudia Simba na Plateau

Saturday December 05 2020
dr tulia pic

MAMBO yamezidi kunoga huko kwa mkapa. Hiyo ni baada ya Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania, DkTulia Ackson kutua uwanjani kushuhudia mchezo wa hatua ya awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika Kati ya Simba na Plateau  United ya Nigeria.

Simba inaikaribisha Plateau United katika mchezo wa marudiano utakaoanza saa 11:00 jioni kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mchezo wa kwanza uliofanyika nchini Nigeria, Simba iliishinda bao 1-0 lililofungwa na Clatous Chama. Tulia amefika saa 10:16 jioni na kupokelewa na Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa timu hiyo Mohammed Dewji 'Mo' ambaye nae alikuwa amewasili muda huo.

Baada ya wote kushuka kwenye magari yao yaliyowaleta uwanjani  walipeana mikono Kisha kuongozana kwenda katika eneo la VIP ambalo ndilo hukaa wageni mashuhuri. 
Dkt Tulia ni mmoja wa mashabiki kindakindaki wa Simba.
Na Olipa Assa na Oliver Albert

Advertisement