Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tukutane palepale muone shoo tamu, Berkane waingia ubaridi

KITENDO cha Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuipa Simba nafasi ya kuingiza mashabiki 35,000 katika pambano lao la leo dhidi ya RS Berkane, imewapa mzuka mashabiki na kuitana Kwa Mkapa kupata shoo tamu ya mabao.

Aidha nahodha msaidizi wa timu hiyo, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ amesema kurejea kwa wenzao waliokosekana kwenye mechi zao mbili za ugenini za michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika imewaongeza mzuka.

Simba leo itakuwa wenyeji wa Berkane kutoka Morocco, huku ikipewa nafasi na CAF kuingiza mashabiki 35,000 ambao ni nusu ya wale wanaoingia katika Uwanja wa Benjamin Mkapa wenye uwezo wa kubeba mashabiki 60,000.

Kitendo hicho kimewapa mzuka zaidi mashabiki na wanachama wa klabu hiyo walioitana kwenda kuwavuruga Wamorocco walioitungua timu yao mabao 2-0 katika mechi ya kwanza ugenini wiki iliyopita.

Mwanachama lialia wa Simba, Justin Joel aliliambia Mwanaspoti, fursa hiyo waliyopewa katika kila mechi za Kimataifa inawapa nafasi ya kuwashuhudia nyota wao wakiwa katika mapambano, hivyo wajitokeze kwa wingi.

“Simba ndio wanatamba kwa sasa Tanzania, hivyo huu mchezo ni muhimu sana, sisi tunawaomba mashabiki wawe wa Simba na hata majirani zetu waje kwa wingi tutumie vyema nafasi hizo ambazo tumezipata,” alisema.

Big Simba mkali wa Chalinze alisema, anaimani kubwa na kikosi chao kuelekea mchezo wa leo, lakini kikubwa akiwataka wachezaji kuhakikisha wanapambana kutumia vyema dakika 90.

“Sio mechi ndogo ni kubwa na kila timu inahitaji matokeo kupata pointi tatu, ila tunaimani kubwa na wachezaji wetu watatupambania na sisi ni jukumu letu kwenda kuwaongeza morali kwa shangwe zetu,” alisema.


MSIKIE ZIMBWE

Nahodha msaidizi wa Simba, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ amesema kurejea kwa wenzao ni faida kwa timu yao na anaamini wataishukia Berkane wakiwa na hasira ili kulipa kisasi cha kipigo cha ugenini.

Kibu Denis, Chris Mugalu, Sadio Kanoute, Jonas Mkude, Shomary Kapombe na Aishi Manula wote wamerejea kikosini baada ya kulikosa pambano la Morocco na Tshabalala alisema; “Mchezo ni mgumu, ila tunamshukuru wenzetu waliokuwa majeruhi wamerejea na kuongeza nguvu zaidi kikosini.”

Tshabalala alisema, kila mchezaji amepania kuibeba timu ili ishinde mchezo huo kwa nia ya kujiweka pazuri katika msimamo na kutimiza lengo lao la kufuzu hatua ya robo fainali ikiwa ni rekodi kwao kama timu ya Tanzania.

Hakuna timu ya Tanzania katika Kombe la Shirikisho linalochezwa kwa mfumo wa sasa kufika robo fainali, licha ya Yanga kucheza makundi mara mbili 2016 na 2018 na Namungo msimu uliopita.