Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Torres: Apoteza fedha kwa kukimbia benchi

Fernando Torres.

Muktasari:

Lakini, hofu ya benchi imemkimbiza na kumfanya akubali kupoteza Pauni 115,000 baada ya kuamua kwenda kucheza kwenye Ligi ya Serie A ambapo miaka yake miwili atakayodumu San Siro atakuwa akilipwa Pauni 60,000 tu kwa kila wiki. Ni pesa kidogo kwa mchezaji wa aina yake.

BORA kuwa nacho kuliko kukosa kabisa. Stamford Bridge alihesabika kama mmoja wa wachezaji matajiri wanaocheza kwenye Ligi Kuu England kutokana na akaunti yake ya benki kuingizwa Pauni 175,000 kila wiki.

Lakini, hofu ya benchi imemkimbiza na kumfanya akubali kupoteza Pauni 115,000 baada ya kuamua kwenda kucheza kwenye Ligi ya Serie A ambapo miaka yake miwili atakayodumu San Siro atakuwa akilipwa Pauni 60,000 tu kwa kila wiki. Ni pesa kidogo kwa mchezaji wa aina yake.

Hata hivyo, Pauni 60,000 anazolipwa kila wiki ni nyingi kwa wachezaji wa AC Milan, kwa sababu yeye ndiye anayelipwa pesa nyingi zaidi katika timu hiyo kutokana na viwango vya mishahara vilivyotolewa kwa msimu huu.

Unataka kumjua ni nani, ni Fernando Torres. Ameona potelea mbali kukosa Pauni 115,000 kwa wiki, lakini si kwa kuendelea kunyanyasika kwenye benchi na kuwashuhudia wenzake Diego Costa na ‘babu’ Didier Drogba wakitesa kwa kupangwa klabuni Chelsea. Ameamua kuondoka zake kwa sababu pesa si kila kitu kwake.

Anavyopata kipato

Straika huyo aliyezaliwa Machi 20, 1984 huko Fuenlabrada, Hispania chanzo kikubwa cha kipato chake kimetokana na mchezo wa soka. Kimo chake cha futi 6 na inchi 1 kimempa dili nyingine pia za masuala ya mitindo ambazo zwimemwongezea pesa katika maisha yake.

Kwenye klabu ya Chelsea, Torres alikuwa akivuna Dola 17 milioni kwa mwaka kutokana na malipo ya mishahara yake.

Ubora wake uwanjani ulimfanya abambe dili nyingi nzuri za udhamini zinazomwingiza Dola 3 milioni. Kampuni kubwa zinazomdhamini mwanasoka huyo ni Adidas na PepsiCo. Lakini, amekuwa akijihusisha pia na upigaji wa picha mbalimbali za kupamba majarida.

Ana mkataba pia na kampuni ya Pro Evolution ambayo kwa pamoja na Pepsi na Adidas zinamfanya aweke kibindoni Dola 3 milioni kwa mwaka. Kutokana na hilo kwa kipindi chote alichokuwa Chelsea, Torres alikuwa akiingiza Dola 20 milioni kwa mwaka. Kwa sasa kiwango hicho kitapungua kutokana na mshahara wake anaolipwa Rossoneri kuwa wa chini sana. Mwaka 2009, Torres aliripotiwa kuingiza kiasi cha Pauni 14 milioni.

Makazi na magari ya kifahari

Kutokana na kutengeneza pesa za kutosha, Torres amewekeza kwa makazi bora na kuendesha magari ya thamani kubwa.

Jarida la Forbes lilibainisha kwamba kwa mwaka mmoja, Torres aliingiza Dola 20 milioni na hilo limempa jeuri ya kuwa na makazi ya maana na kumiliki usafiri wenye hadhi yake.

Ukiweka kando nyumba zake za Madrid, London staa huyo ana mjengo wa nguvu huko kwenye maeneo ya Woolton. Kwa upande wa magari, kwenye gereji yake Torres ana ‘ndinga’ za maana na baadhi ya usafiri wake wa kifahari anaomiliki ni Aston Martin DBS na Mercedes-Benz M-Class.

Maisha ya mapenzi

Torres alifunga pingu za maisha na mrembo Olalla Dominguez Liste, ambaye alikuwa na uhusiano naye tangu 2001. Harusi yao ilifanyika Mei 27, 2009 ilikuwa ya kawaida sana na wageni wawili tu waliokuwa wamealikwa katika sherehe.