Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Timu ya Mlandege yatwaa ubingwa Ligi Kuu Zanzibar

MLANDEGE Pict

Muktasari:

  • Mechi hiyo imehitimisha michezo 30 ya mzunguko wa ZPL na Mlandege, alitwaa ubingwa kwa idadi ya mabao 48,katika mchezo huu Abdallah Iddi aliipatia Mlandege bao la kwanza katika dakika ya 15, na bao la pili dakika ya 44.

Timu ya Mlandege imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu Zanzibar (ZPL) kwa msimu wa 2024-25 baada ya kuitandika New City mabao 4-2.

Mechi hiyo imehitimisha michezo 30 ya mzunguko wa ZPL na Mlandege, alitwaa ubingwa kwa idadi ya mabao 48,katika mchezo huu Abdallah Iddi aliipatia Mlandege bao la kwanza katika dakika ya 15, na bao la pili dakika ya 44.

Huku Said Khamis Matola akiipatia timu hiyo mabao mengine mawili kabla ya mchezo kumalizika na New City ikipata mabao mawili ya kufutia machozi dakika za jioni za mchezo huo.

Pia, Katika mchezo huo, Abdallah Iddi Pina ameibuka man of the Match katika mchezo huo.

Kwa upande mwengine, KVZ imechukua nafasi ya pili baada ya kuifunga timu ya Kipanga  bao 1-0 ikivuna alama 62 na kujipatia mabao 23.