TFF yaomba radhi kuahirishwa mechi ya Simba, Yanga

Sunday May 09 2021
kuahirishwa pic
By Zourha Malisa

Dar es Salaam. SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeomba radhi kwa wadau wa soka nchini kutokana na kitendo cha kuahirishwa mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga, huku ikiitaka Bodi ya Ligi kutoa taarifa ya kina kuhusu kuahirishwa kwa mchezo huo.

TFF jana Jumamosi Mei 8, 2021 ilitoa taarifa ya kusogeza mbele muda wa mechi ya Simba dhidi ya Yanga na taarifa hiyo ilieleza mechi hiyo kuanza saa 1 usiku badala ya saa 11 jioni iliyopangwa awali.

kutua pic 1

Baadaye, Bodi ya Ligi litangaza kuahirisha mechi hiyo ya Ligi Kuu Tanzania Bara ya dabi ya Kariakoo, Simba na Yanga iliyokuwa ichezwe  katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

SIMBAA PIC

Kwa mujibu wa taarifa ya TFF iliyotolewa leo Jumapili Mei 9, 2021, imeeleza kuomba radhi wadau wa soka na kutoa maelekezo kwa Bodi ya Ligi itoe taarifa ya kina kuhusu kuahirishwa kwa mchezo huo sambamba na kushughulikia viingilio vilivyolipwa na mashabiki na wadau wa soka.

Advertisement
mabomu pic

“Tunawaomba wapenzi wa mpira kuwa watulivu wakati jambo hili linashughulikiwa kwa haraka kwa taratibu za kikanuni, lakini huku tukishirikiana kwa karibu na wadau wote ikiwemo Serikali,” imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa jambo hilo linaendelea kushughulikiwa kikanuni, kufanya vikao mbalimbali, pia itakutana na klabu hizo mbili Simba na Yanga

Advertisement