Mashabiki Simba, Yanga wapigwa mabomu

Saturday May 08 2021
mabomu pic
By Thomas Ng'itu

ASKARI wa Jeshi la Polisi Tanzania wametumia mabomu ya machozi kuwasambaratisha mashabiki waliojitokeza katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Askari hao imebidi kutumia mabomu hayo baada ya mashabiki wote (Simba na Yanga) kusikika wakidai kurejeshewa pesa zao.

Mashabiki hao walikuwa wanazunguka katika sehemu ya kukaa magari wakiwa wamechanganyika Simba na Yanga huku magari yakiwa yanashindwa kutoka uwanjani.

Hali hiyo iliwalazimu maaskari kutumia mabomu ndani na nie ya uwanja kukimbiza mashabiki na hali ikawa tulivu.

Baada ya mashabiki kuondoka, polisi walikuwa wanazunguka kila kona kuangalia watu waliokuwa wamekaa karibu na magari na kutaka kujitambulisha.

Advertisement