TFF yabariki vijana FC Vito Singida kwenda Finland

Muktasari:
FC Vito Singida ni timu yetu ya kwanza kwenda nje, michezo mikubwa barani Ulaya, wana umri 10 mpaka 12, Helsinki Cup yatakayoanza tarehe 8 mpaka 13.
Dar es Salaam. Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limebariki vijana wa timu ya Fc Vito Singida kwenda nchini Finland katika Mashindano ya Helsinki yanayoshirikisha vijana wenye umri chini ya miaka 10 mpaka 12.
Akizungumza makao makuu ya ubalozi wa Finland nchini, Mkurugenzi wa Ufundi TFF, Oscar Mirambo alisema vijana hao waitumie fursa hiyo kwaajili ya kujifunza zaidi.
"Hii ni fursa hampaswi kucheza kama shughuli ya kuchangamsha mwili, naamini mtaendelea kujifunza kupitia wenzenu na mnatakiwa msiwe wapweke, lakini muwe na nidhamu," alisema.
Aliongeza kwa kuwaambia "Nendeni mkacheze na mfurahie mpira, tunaamini kabisa kwamba mnaenda na mtarudi na kikombe".
Meneja wa Mradi wa Tanzania Teachers Union (TTU), Mwalimu Noel Bugado alisema lengo la kwenda katika mashindano hayo ni kutengeneza timu ya taifa ya baadaye.
"Tunapotaka kuwa na timu yenye wachezaji wazuri lazima tuanzie huku chini, hata kwa timu yetu iliyopo Afcon tumeona walichokipata kwahiyo sisi tunawaandaa ili waje kuwa wachezaji wazuri kwa baadae.
Wachezaji wanaoondoka, Fred Edson, Jovin Kabeya, Philipo Mwigema, Samson Jackson, Simon Bugado, Raphael Raphael, Asajile Lisu, Hudhaifa Kweka, Omari Ismail, Elia Makhata, Kelvin Tikae na Maregesi Dominick. Mwalimu Mohammed Kweka.