TFF kuziondoa Simba, KMC Uwanja wa Uhuru

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeufungia uwanja wa Uhuru kutumika kwa michezo ya Ligi Kuu kutokana na kukosa vigezo vya kikanuni na Sheria ya mpira wa miguu.
Taarifa hiyo imetolewa na TFF leo Desemba 21 na Ofisa Habari na Mawasiliano, Clifford Ndimbo imeeleza kuwa "Miundombinu ya uwanja huo haikidhi matakwa ya kanuni kama ilivyoainishwa kwenye masharti ya kanuni ya leseni za klabu"
TFF imezitaka timu zote zinazotumia uwanja huo kwa michezo yao ya nyumbani kulazimika kutumia uwanja mwingine kama kanuni inavyojielekeza mpka uwanja wao utakapofunguliwa, baada ya kufanyiwa marekebisho na kukaguliwa na TFF.
Uwanja wa Uhuru unatumika na Simba na KMC kama uwanja wa nyumbani na kwa Championship ni Cosmopolitan, Pan Africans na Green Warriors.
KMC inatarajiwa kucheza dhidi ya Simba kesho Desemba 22 katika Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.