Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TFF: Fei Toto ni mchezaji wa Yanga

Muktasari:

  • kwa mujibu wa taarifa hiyo Feisal Salim bado ni mchezaji wa Yanga na anapaswa kufanya majadiliano na Klabu kabla ya kuvunja Mkataba

KAMATI ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imefutilia mbali shauri la kiungo wa Yanga Feisal Salim leo Machi 6, 2023.

Taarifa hiyo inasema "Awali Kamati ya Sheria na Hadhi ya wachezaji ilisikiliza malalamiko hayo kwa njia ya maandishi amabapo pande zote (Young Africas na Feisal Salim) ziliwakilishwa na wansheria wao ambao walipewa pia muda wa nyongeza wa kufafanua walichowasilisha kwenye majumuisho yao ya maandishi"

"Baada ya kupitia na kutafakari kwa kina hoja zote za pande husika, kamati imetupilia mbali maombi hayo kwa msingi kwamba ilishaamua juu ya uhalali wa Mkataba wa mchezaji huyo na klabu yake kwamba ana Mkataba unaoendelea mpaka 2024"

kwa mujibu wa taarifa hiyo Feisal Salim bado ni mchezaji wa Yanga na anapaswa kufanya majadiliano na Klabu kabla ya kuvunja Mkataba

Fei aliondoka Yanga kuanzia mwishoni mwa mwaka jana, baada ya kudai kuwa anahitaji maslahi zaidi, akavunja mkataba kwa kuweka kiasi cha Sh112 milioni kwenye akaunti ya klabu hiyo, lakini baadaye Kamati ya Sheria Hadhi za Wachezaji iliyopo chini ya Shirikisho la Soka Tanzania TFF, ilisema kuwa mchezaji huyo bado ni mali ya Yanga kwa kuwa hakufuata taratibu za kuvunja mkataba huo.