Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TETESI ZA USAJILI BONGO: Samatta kumfuata Msuva Saudia

Muktasari:

  • Kama dili hilo litakamilika huenda Samatta akakutana na pacha anayecheza naye Taifa Stars, Msuva anayeichezea Al Najma katika ligi hiyo.

NYOTA wa kimataifa wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa katika timu ya PAOK ya Ugiriki, Mbwana Samatta ‘Popat’ inadaiwa anajiandaa kumfuata Saimon Msuva anayecheza soka nchini Saudia Arabia baada ya klabu ya Al Kholood iliyopanda  Ligi Daraja la Pili nchini humo kutuma maombi ya kumtaka nahodha huyo wa Taifa Stars kwa mkopo.                                         

Kama dili hilo litakamilika huenda Samatta akakutana na pacha anayecheza naye Taifa Stars, Msuva anayeichezea Al Najma katika ligi hiyo.

Samatta amekuwa na wakati mgumu wa kupata nafasi ndani ya kikosi cha PAOK na mkataba alionao na Wagiriki hao unatarajiwa kutamatika Juni, mwakani.