Tembo Warriors yatakata Canaf 2021

Saturday November 27 2021
Warriors PIC
By Leonard Musikula

Timu ya Taifa ya Tanzania  kwa watu wenye ulemavu 'Tembo Warriors' imeanza kwa kishindo mashindano ya Bara la Afrika ya soka kwa watu wenye ulemavu 'Canaf' kwa kuifunga timu ya taifa ya Morocco mabao2-1.

Dakika 25 za kipindi cha pili zimewatosha kuondoka na ushindi huo baada ya kipindi cha kwanza kukubali kufungwa bao moja kwa sifuri

Mabao ya Tembo warriors yamefungwa na mshambuliaji wao Alfani Kiyanga pamoja na nahodha wao Juma kidevu na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa mabao 2-1.

Akizungumza na Mwanaspoti kocha wa Tembo warriors Salvatory Edward amesema kuwa siri ya ushindi huo ni maandalizi mazuri

"Kipindi cha kwanza tulipoteza umakini na wapinzani wetu wakatumia hiyo nafasi na wakapata bao la kuongoza"

 "Lakini kipindi cha pili tukarejea na kuongeza umakini zaidi na hatimaye tukasawazisha mabao hayo ila kiujumla ni maandalizi mazuri pamoja na kujituma kwa wachezaji" anasena Salvatory.

Advertisement

Ushindi huo unaifanya Tembo Warriors kuongoza kundi A wakiwa na alama tatu

Advertisement