Tanzania yanukia kombe la Dunia

Tanzania yanukia kombe la Dunia

Timu ya taifa ya Wanawake kwa umri chini ya miaka 17, imeanza vizuri kampeni yake ya kuwania kushiriki kombe la Dunia mwaka huu huko India.

Tanzania imeanza kampeni hiyo dhidi ya Botswana katika mchezo wa mkondo wa kwanza ambao umepigwa katika Uwanja wa Amani Visiwani Zanzibar na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 7-0.

Mabao ya Tanzania yalifungwa na Neema Paul aliyeingia kambani mara mbili sawa na Clara Luvanga, huku Aisha Juma akifunga "hat trick" iliyokamilisha mvua hiyo ya mabao.

Baada ya mechi hiyo mabinti hao watasafiri hadi nchini Botwasana kwa ajili ya mchezo wa marudiano utakaopigwa Machi 20 mwaka huu.

Ikiwa itafanikiwa kushinda na kuvuka hatua hiyo, Tanzania itakuwa na kibarua cha kupambana na kwenye hatua ya tatu na baada ya kuvuka itaenda hatua ya nne ambayo ni yamwisho.

Kwenye hatua hiyo ya nne timu sita zitakutana ambapo zitacheza mechi za nyumbani na ugenini ili kuzipata timu tatu zitakazosafiri kwenda India kuiwakilisha Afrika kwenye mashindano ya kombe la Dunia yatakayoanza Oktoba 11 hadi 30.