Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzania yakumbushwa kujipanga Olimpiki 2028

Olimpiki Pict
Olimpiki Pict

Muktasari:

  • Michezo hiyo ijulikanayo kama LA 2028 itaanza Julai 14-30 mjini Los Angeles,  Marekani.

MAKATIBU wakuu wa vyama vya michezo vinavyoshiriki Olimpiki wametakiwa kuanza kuweka mikakati ya maandalizi ili timu zao ziweze kushiriki kwenye Olimpiki ya 2028.

Michezo hiyo ijulikanayo kama LA 2028 itaanza Julai 14-30 mjini Los Angeles,  Marekani.

Akizungumza wakati wa kufungua semina ya makatibu wakuu wa vyama vya Michezo iliyo kwenye programu ya Olimpiki, rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Gulam Rashid amesema ili kushiriki michezo hiyo ni lazima kufikia viwango vya kimataifa.

"Kama hauna ushirikiano na Chama cha mchezo wako wa kimataifa ni ngumu kuweza kufikia viwango vya Olimpiki," amesema Gulam.

Katika semina hiyo ambayo ilishirikisha makatibu wakuu wa vyama vya michezo zaidi ya 20, Gulam amesema makatibu wakuu ndiyo watendaji kwenye vyama au mashirikisho ya michezo.

"Rais ni mtu wa sera, ninyi makatibu wakuu ndiyo watendaji, tunafahamu kuna Olimpiki 2028, hivyo tunahitaji kuweka mikakati mapema ya maandalizi," amesema Gulam.

Awali Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi alisema kabla ya Olimpiki 2028 kuna michezo ya Afrika na Michezo ya Jumuiya ya Madola ambako huko Tanzania pia inashiriki.

"Mashindano haya na yale ya vyama au mashirikisho yenu ya kimataifa ikiwamo ya dunia na kanda ni muhimuvkushiriki ili kufikia viwango vya kufuzu Olimpiki ijayo," amesema.

Mkufunzi katika semina hiyo Henry Tandau aligusia mada mada mbalimbali zilizotolewa kwa matibu hao ikiwamo ya uongozi na utawala bora katika michezo, mtandao wa Olimpiki na nyinginezo.

Tanzania imeanza kushiriki Olimpiki mwaka 1964 wakati huo ikijulikana kama Tanganyika, imeendelea kushiriki hadi sasa ikiwa na rekodi ya medali mbili za fedha za riadha kwenye michezo ya 1989, Moscow Russia.