Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tangulia Ruge, huenda Simba, Yanga zikaamka kupitia kwako

Muktasari:

Kuna makato ya kushangaza wakati mwingine unashindwa kujua inakuwaje taasisi ambazo hazina michango yoyote kwa timu shiriki.

MAISHA si lolote. Maisha ni udanganyifu tu. Yaani leo ulikuwa unaoga mwenyewe. Unavaa nguo uzitakazo. Unajiendea utakako na kupanda usafiri unaouchagua mwenyewe na hata kulala ndani ya nyumba kubwa kuliko maumbile uliyonayo na kulala katika kitamba kizuri.

Lakini ghafla kila kitu unafanyiwa. Unabebwa kwenye usafiri dhalili wa jeneza. Unaenda kulazwa kwenye shimo lenye kiza. Lisilo la liyoyozi wala taa. Mauti. Mauti yanatisha na ni mawaidha kwa watu wenye akili. Ruge Mutahaba amekwenda. Kesho tukijaliwa atakuwa akihifadhiwa kwenye nyuma yake ya milele kule Kagera. Inaumiza. Inasikitisha.

Ndio maisha yalivyo, maadam umejikuta hai duniani, basi jua kabisa kuna siku utakuwa maiti.

Mungu Aiweke Mahali Pema Roho ya Ruge. Atakumbukwa kwa yote aliyoyafanya ndani ya jamii ya Kitanzania. Tumuenzi kwa mazuri aliyoyafanya enzi za uhai wake na kumuombea katika safari yake kwa kukumbuka kua Kila Nafsi lazima ionje mauti na Hakika sisi ni Allah SW na Kwake tutarejea!

Tukiachana na msiba huo mzito uliogusa mioyo ya Watanzania walio wengi kwa namna marehemu Ruge enzi za uhai wake anatajwa hakupenda kufeli. Hakuridhika kirahisi na alikuwa mbishi kwelikweli wa kupambania mafanikio kiasi wakati mwingine kuwakwaza wengine.

Namna alivyokuwa akijua kuangalia fursa na kuhakikisha anafanikisha lake, ni vyema hata klabu za Simba na Yanga nazo zikajifunza kwake katika kuepukana na ‘unyonyaji’ wanaoulazimisha kufanyiwa kwa kushindwa kutumua fursa ya ukubwa wa majina yao katika soka la Tanzania.

Ndio, baadhi ya wadau wa soka wanashangaa. Klabu nazo zinashangaa na kulalamika chini kwa chini. Bahati mbaya wanashindwa kusema hadharani, labda ni kwa vile walikubaliana mapema kabla ya Ligi Kuu Bara kuanza msimu huu na hata misimu mingine ya nyuma iliyopita.

Tunazungumzia suala la mgao wa mapato ya mlangoni katika mechi za Ligi Kuu. Klabu zimekuwa zikinyonywa waziwazi. Fedha zinazopatikana kwenye mechi husika zinakuwa nyingi lakini mgao unaofanyika unaziacha klabu zikiambulia vijisenti, huku taasisi nyingine zikibeba fedha nyingi. Baadhi ya mechi za Ligi Kuu zimekuwa zikiingiza kiasi kikubwa cha fedha, lakini inachopata klabu husika ni kidogo kiasi cha kushangaza.

Kuna makato ya kushangaza wakati mwingine unashindwa kujua inakuwaje taasisi ambazo hazina michango yoyote kwa timu shiriki.

Kwa mfano pambano la watani limeingiza zaidi ya Sh 343 milioni, lakini klabu mwenyeji yaani Yanga imeambulia Sh165 milioni, huku zilizobaki zikiwa ni zaidi ya nusu ya fedha zilizoingizwa kwenye pambano hilo zikienda kwingine walioorodheshwa kwenye mgao huo.

Ni kama vile klabu zimegeuzwa kama chuma ulete.

TFF inavuna fedha, TPLB inavuna fedha, BMT inavuna fedha mpaka DRFA ambayo mpaka sasa ni ngumu kujua shughuli zake hasa baada ya wilaya za jijini la Dar es Salaam kutambulika kama Mikoa kisoka nayo pia inavuna fedha.

Na mambo mengine ambayo yote ni kutengeneza mazingira ya kuvuna fedha, kupitia klabu zinazoendeshwa kwa gharama kubwa bila ya kusaidiwa pale zinapokwama!

Ndio maana watu wanashangaa. Klabu zinashangaa na kulalamika, lakini wanaonufaika kwa migongo ya klabu wala hawapigi kelele wala kunung’unika.

Mechi ya Simba na African Lyon iliyopigwa Arusha iliingiza kiasi cha Sh 55.6 milioni, wenyeji Lyon wakaambulia Sh 26 milioni, kiasi cha Mmiliki wake, Rahim Kagenzi ‘Zamunda’ alishindwa kuvumilia na kusema wazi alichokiingiza kulinganisha na gharama walizotumia kuelekea mchezo huo ni kama hasara kwao.

Hata hivyo, ishu hapa sio TFF, BMT, DRFA ama Selcom ama TPLB, bali ni klabu zenyewe hasa klabu kubwa za Simba na Yanga. Zimekubali kunyonyeka wakati walikuwa na nafasi ya kuepuka kugeuzwa mipira ya kuwanufaisha wengine.

Simba na Yanga na umri wao wa miaka zaidi ya 80 hazina viwanja kama African Lyon. Azam iliyoanzishwa miaka 10 iliyopita tayari ina uwanja wenye hadhi na unaotambuliwa na CAF, wakati Simba na Yanga wanatangatanga kama digidigi mwituni, kwa vile hazikufikiria mbali.

Leo klabu hizo zinajiandaa kuhama jiji kwenda mikoani kusaka viwanja vya kutumia kwa mechi zao za nyumbani, kisa serikali inavifunga viwanja vyake vya Taifa na Uhuru kwa ajili ya uikarabati kabla ya kuanza kwa michuano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana U17.

Yanga ingekuwa na Uwanja, mathalani Kaunda ungekuwa umejengwa na kutumika kwa ligi, makato yasingewaumiza sijui wamiliki wa uwanja, gharama za mchezo na mengineo, wangebeba wenyewe kama klabu. Lakini kwa kuwa wenyewe walijichanganya wacha walizwe!

Simba walioingia kwenye mfumo wa kisasa hivi karibuni, hawachekani na Yanga, hawana uwanja wao licha ya kutamba kama klabu yenye fedha na ufadhili mnono. Wamlaumu nani?

Klabu hizi zinajikosesha mapato wenyewe kwa sababu hawakufikiria mbali. Walifikiria wala kujifunza kwa klabu za barani Ulaya ambazo hata za uchochoroni huwa na viwanja vyao. Viwanja vya mazoezi hadi vile vya mechi. Klabu kubwa kama Man City, Man United na nyingine Ulaya zinalazimika kuzifuata klabu ndogo kwao na umaamrufu wao, kwa sababu umiliki wa viwanja ni kitu cha kwanza kwa klabu ya kisasa, jambo ambalo Simba na Yanga walilipuuza! Katika pambano la Simba na Yanga la Feb 16, 2019, wamiliki wa Uwanja kwa maana ya serikali ilivuna Sh 41, 303, 948.22 za mgao wa mechi hiyo, huku VAT ikivuna 52,295,338.98, Selcom 15,170,006.25, TFF 13,767,982.74.

Yanga iliambulia Sh165,215,792.86, Gharama za mchezo 19,275,175.83, TPLB 24,782,368.93, BMT 2,753,596.55 na DRFA 8,260,789.64 ikiwa ni sehemu ya mapato yote ya jumla ya Sh 342, 825,000 yaliyoingizwa kwenye pambano hilo la Ligi Kuu.

Ukweli ndivyo ulivyo, kama klabu hazitamka na kujikomboa na wakati mwingine kupiga kelele juu ya marekebisho ya asilimia za mgao wa fedha wanazoingiza kwenye mechi zao za nyumbani zitarajie kuendelea kunyonywa mpaka dahali.

Klabu zinapoteza fedha nyingi kwa vile tu hazina viwanja vyao wenyewe, pia kushindwa kupaza sauti kwa umoja kupigia kelele hii mgawanyo ya fedha iliyoainishwa katika mgao ili kutogeuzwa mirija ya kuneemesha wasiojua uzito wa gharama inazobeba katika maandalizi ya mechi zao