Tanasha wa Diamond ndani ya ‘listening party’ ya AliKiba leo Kenya

Friday October 08 2021
tanasha pic
By Nasra Abdallah

Msanii Tanasha Donna anatarajiwa kuwa moja ya wasanii watakahudhuria shughuli ya kusikiliza albamu mpya ya msanii wa Bongofleva nchini Tanzania, Alikiba inayokwenda kwa jina la ‘Only One King’.

Hilo limebainika leo Ijumaa Oktoba 8, 2021 kupitia ukurasa wa Alikiba ambapo alianika orodha ya wasanii mbalimbali wa Kenya watakaohudhuria hafla hiyo itakayofanyika hoteli ya Trade Mark jijini Nairobi.

Tanasha ambaye ni msanii wa muziki na mtangazaji, ni mzazi mwenziwe na Diamond Platnumz waliojaliwa kupata naye mtoto mmoja katika mahusiano yao kabla hawajaachana.

Ukiacha Tanasha, wapo wasanii wengine akiwemo Khaligraph, Bey T, Nyashinski Otile Brown na mke wa Ben Pal, Anerlisa.

Oktoba 5, Alikiba alizindua albamu yakejijini Dar es Salaam kwa kuwaalika wasanii na watu maarufu mbalimbali nchini Tanzania kuisikiliza kwa mara ya kwanza.

Albamu hiyo inakuwa ni ya tatu kuitoa, ikitanguliwa na ‘Cinderela’ iliyotoka mwaka 2007 na kufuatiwa na ile ya ‘Ali K 4real’ aliyoitoa mwaka 2009.

Advertisement
Advertisement