Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tambwe, Ngoma waiponza Yanga

Muktasari:

Yanga ambayo inatafsiri wa kama klabu yenye kiwango bora cha soka kwa sasa Tanzania na Afrika Mashariki, iliamua kumwaga fungu la maana kuwasajili mastraika hao wa kigeni ili kukabiliana na tatizo la ushambuliaji ambalo limekuwa likizisumbua timu za Tanzania, na ufanisi wa wachezaji hao umeifikisha Yanga kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho ambayo ilikuwa haijafikiwa miaka mingi.


WASHAMBULIAJI, Amissi Tambwe raia wa Burundi na Donald Ngoma raia wa Zimbabwe ambao wanafanya vizuri na Yanga wameiponza timu hiyo na kujikuta ikikosa mshambuliaji yeyote katika kikosi cha Taifa Stars.

Ngoma na Tambwe wameifungia Yanga mabao 38 Ligi Kuu msimu uliopita na kuwa pacha ya ushambuliaji iliyofanya vizuri nchini lakini wameifanya timu hiyo kukosa kabisa mchezaji katika safu ya ushambuliaji ya Stars.

Yanga ambayo inatafsiri wa kama klabu yenye kiwango bora cha soka kwa sasa Tanzania na Afrika Mashariki, iliamua kumwaga fungu la maana kuwasajili mastraika hao wa kigeni ili kukabiliana na tatizo la ushambuliaji ambalo limekuwa likizisumbua timu za Tanzania, na ufanisi wa wachezaji hao umeifikisha Yanga kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho ambayo ilikuwa haijafikiwa miaka mingi.

Uwepo wa wachezaji hao wenye uchu wa mabao umewalazimisha wachezaji wazalendo kusubiri benchi na wakati mwingine kukaa jukwaani kabisa. Wachezaji wa Kitanzania walioshindwa kung’ang’ania namba mbele Tambwe na Ngoma ni Malimi Busungu, Paul Nonda na Matheo Simon. Nonga tayari ameomba kuondoka Yanga ingawa bado uongozi haujamruhusu kwavile ana mkataba wa mwaka mmoja.

Yanga iko kwenye mazungumzo na straika Faty Birori wa Rwanda, tayari kumuongeza kwenye kikosi hicho ingawa habari mbaya ni kwamba mchezaji huyo ambaye kupiga hat trick kwake siyo stori, amefungiwa na CAF na adhabu yake inamalizika mwezi Septemba mwaka huu.

Birori alifungiwa miaka miwili Septemba 2014, baada DR Congo kulalamika kwamba anatumia pasi mbili tofauti za kusafiria na ana majina mawili tofauti lile analolitumia kama raia wa Congo akiichezea Vita Club na lile analotumia akiichezea timu ya Taifa ya Rwanda. Hata hivyo, Wanyarwanda wamempiga chini na akimaliza kifungo chake hatakuwa na timu ya Taifa ya kuichezea kwa vile hawezi kurudi Congo.

Katika kikosi cha Stars kilichofungwa mabao 2-0 na Misri juzi Jumamosi, ni Azam pekee iliyokuwa na mshambuliaji katika kikosi hicho huku Simba na Yanga zikiambulia patupu. Kwa upande wa Azam alianza Farid Mussa.

Yanga baadaye ilifanikiwa kupata mchezaji mmoja katika eneo hilo baada ya Deus Kaseke kuingia akichukua nafasi ya Thomas Ulimwengu katika dakika 10 za mwisho.

Safu ya ushambuliaji ya Stars iliyoanza dhidi ya Misri iliundwa na Farid, Ulimwengu anayecheza soka la kulipwa TP Mazembe, Mbwana Samatta wa KRC Genk ya Ubelgiji na Elius Maguli wa Stand United.

Simba imeponzwa na Hamis Kiiza aliyefunga mabao 19 msimu uliomaliza huku washambuliaji wengine, Ibrahim Ajibu na Mussa Hassan ‘Mgosi’ wakishindwa kumshawishi kocha wa Stars.

Mbali na kukosa washambuliaji, Yanga ilifanikiwa kuingiza wachezaji watatu katika kikosi cha kwanza cha Stars ambao ni Juma Abdul, Deo Munishi ‘Dida’ na Haji Mwinyi huku Simba ikiwa na Mwinyi Kazimoto pekee katika kikosi hicho.


KOCHA ANENA

Kocha wa zamani wa Taifa Stars, Mshindo Msolla alisema Saimon Msuva wa Yanga alistahili kuwepo katika kikosi hicho kutokana na kufanya vizuri katika mechi za kimataifa huku akikosoa uamuzi wa kocha wa Stars, Boniface Mkwasa kumuanzisha Haji Mwinyi.

“Inategemea pia wachezaji gani wameanza katika eneo hilo la ushambuliaji, Azam walikuwa na Farid ila ni kweli Simba na Yanga zilikosa hata mmoja, kwa upande wa Yanga wangeweza pia kuwa na Msuva ambaye katika mechi za kimataifa za Yanga alifanya vizuri, ana utimamu wa mechi japo wakati mwingine anakosa uwiano mzuri wa kiwango chake.

“Sifahamu kwanini John Bocco alipewa nafasi, hana kiwango kizuri anapocheza mechi za kimataifa, kiwango chake kimeishia tu hapa ndani, anafahamu namna ya kuwafunga mabeki wa Tanzania tu,”alisisitiza Msolla ambaye ndiye kocha msomi zaidi nchini.