Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Taifa Stars kamili kila idara kuichakaza Burundi Uwanja wa Taifa

Muktasari:

Hakuna sababu kwa Stars kuingia kwa presha kubwa ya kutafuta ushindi, hivyo bado iko haja ya kupanga kikosi na mbinu zitakazokuwa na uwiano mzuri kwenye kushambulia na kuzuia.

NI mechi inayohitaji hesabu kali za kimbinu kwa benchi la ufundi na wachezaji wa Stars ili kukamilisha lengo la kuitupa nje Burundi.
Hesabu kubwa za Burundi bila shaka zitakuwa ni kwenye kusaka bao/mabao ya mapema kwa lengo la kutibua mipango na kuipa mzigo mkubwa Stars ikiwa nyumbani.
Hakuna sababu kwa Stars kuingia kwa presha kubwa ya kutafuta ushindi, hivyo bado iko haja ya kupanga kikosi na mbinu zitakazokuwa na uwiano mzuri kwenye kushambulia na kuzuia.
Eneo ambalo Stars inapaswa kuwa makini zaidi na kutafuta namna ya kuhakikisha halileti madhara ni upade wa walinzi wa pembeni ambako ndiko nguvu ya Burundi ilipo.
Burundi inategemea zaidi mashambulizi ya pembeni na ndiko kulizalisha bao lao pekee kwenye mchezo wa kwanza uliofanyika Bujumbura, siku tano zilizopita.
Winga Mohamed Amissi anayechezea Heracles ya Uholanzi anapaswa kuchungwa zaidi na Stars kwani ndiye aliyekuwa uti wa mgongo katika ujenzi wa mashambulizi ya Burundi katika mechi iliyopita.
Amissi mwenye umri wa miaka 19, ana uwezo wa hali ya juu katika kumiliki mpira, kupiga chenga na pasi zinazowafikia walengwa kwa usahihi pamoja na kupenya ukuta wa timu pinzani, hivyo mabeki wawili wa Stars watakaocheza upande wa pembeni wamchunge vilivyo.
Pia kuna winga mwingine, Bienvenue Kanakimana ambaye ana sifa zinazoshabihiana na zile za Amissi akiwa na umri wa miaka 19.
Lakini kuna washambuliaji wa kati, Fiston Abdoulrazack, nahodha Saido Berahino na Cedric Amissi ambao nao wanapaswa kuchungwa kutokana na kasi, nguvu na uwezo wa kufumania nyavu walionao sambamba na kutengeneza nafasi.
Pamoja na kucheza kwa tahadhari kubwa kwenye safu ya ulinzi hasa pembeni, Stars inapaswa kuhakikisha inakamata safu ya kiungo kama ilivyokuwa katika dakika 45 za kwanza za mechi iliyopita.
Pamoja na kupata bao moja kwenye mechi ya ugenini, safu ya ushambuliaji ya Stars inapaswa kuongeza utulivu na umakini katika kutumia nafasi za mabao ambazo itatengeneza katika kufumania nyavu.
Kwenye mechi iliyopita, Stars ilipoteza baadhi ya nafasi kama ile iliyopotezwa na Saimon Msuva katika dakika ya 17 ya mchezo.
Msuva alipoteza nafasi muhimu ya kuifungia bao akiwa anatazamana ana kwa ana na kipa Jonathan Nahimana ambapo alipiga shuti lililombabatiza ingawa baadaye kipindi cha pili alifunga bao la kusawazisha mnamo dakika ya 84. Baada ya kupata muda wa kutosha kufanya mazoezi ya pamoja na timu, beki wa Nkana FC, Hassan Kessy anaweza kuanza nafasi ya beki wa kulia badala ya Haruna Shamte ambaye alionekana kupwaya kwenye mechi ya kwanza.
Zaidi ya hilo, hakuonekani kama kunaweza kuwa na mabadiliko makubwa ingawa pia upo uwezekano wa winga wa CD Tenerife, Farid Musa kuanza kama mbadala wa Hassan Dilunga.

Kila mmoja
anataka ushindi
Kocha msaidizi wa Tanzania, Juma Mgunda anasema wanatambua umuhimu wa mchezo huo na wamejipanga kuhakikisha wanapata matokeo mazuri wakiwa katika uwanja wa nyumbani.
“Kiufundi tupo vizuri na upungufu ulioonekana tumeufanyia kazi na mazuri yaliyoonekana tayari tumeyaongezea,” alisema.
Nahodha msaidizi wa Stars, Himid Mao anasema, “katika mpira presha haiepukiki lakini kama wachezaji tunaichukulia kama changamoto, tunaamini presha hiyo itatufanya kuinjoyi na kupata matokeo.”
Kwa Burundi, Olivier Niyungeko anasema, “tuna nafasi bado ya kusonga mbele licha ya kwamba matokeo sio mazuri sana kwetu, tumewaona namna ambavyo Tanzania wanacheza na tayari tumefanyia kazi.”
Akizungumzia kukosekana kwa wachezaji wake, Jules Ulimwengu na Laudit Mavugo anasema hilo haliwezi kuathiri katika kikosi chake.
“Wachezaji wote niliokuja nao ni wazuri, nawaamini na kila kitu kitaenda sawa na hawa ambao wamebaki naamini tunaweza kukutana nao hatua inayofuata,” anasema.