Tabarez: Suarez hatafanya kituko

Suarez alifungiwa kushiriki masuala yote ya soka kwa miezi minne baada ya tukio lililotokea miaka minne iliyopita nchini Brazil.
Mshambuliaji huyo wa Barcelona ataonekana leo uwanjani Saa 9:00 alasiri akiiongoza nchi yake ya Uruguay dhidi ya Misri.
"Kilichotokea Brazil ni sehemu ya maisha na wazi limekuwa ni somo kubwa kwake lilobadilisha maisha yaje," alisema Tabarez.
Japokuwa Suarez alinusurika kupewa kadi nyekundu kwa kumng’ata, hakuweza kucheza mechi inayofuata ya Uruguay waliofungwa 2-0 na Colombia katika hatua ya 16 bora.
Miaka minne kabla ya kutukio la kung’ata, Suarez aliingia katika vichwa vya habari baada ya kudaka mpira katikati ya goli na kusababisha apewe kadi nyekundu katika mchezo wa robo fainali dhidi ya Ghana.
Hata hivyo, Tabarez anaamini nyota huyo mwenye miaka 31, ataonyesha uwezo wake wakati Uruguay ikitaka kushangaza watu Russia.
Suarez kinara wa ufungaji wa muda wote wa Uruguay atashirikiana na Edinson Cavani kuongoza mashambulizi dhidi ya Misri kwenye Uwanja wa Yekaterinburg.