Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aucho, Mukwala wachemsha Uganda

MUKWALA Pict

Muktasari:

  • Tuzo hizo zilizofanyika Mei 30, chini ya Shirikisho la Soka Uganda (FUFA), Aucho na Mukwala waliangushwa Rodgers Mato, aliyeibuka mshindi.

KIUNGO nyota wa Yanga, Khalid Aucho na mshambuliaji wa Simba, Steven Mukwala wamechemsha huko Uganda baada ya kushindwa kubeba tuzo  tuzo za mashabiki kwa wachezaji wanaocheza nje.

Tuzo hizo zilizofanyika Mei 30, chini ya Shirikisho la Soka Uganda (FUFA), Aucho na Mukwala waliangushwa Rodgers Mato, aliyeibuka mshindi.

Mato ambaye ni mshambuliaji anayeichezea klabu ya Vardar ya Marcedonia Kaskazini, inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.

Katika kipengele hicho,  Aucho, Mukwala na Mato walikuwa wakichuana na Elio Capradossi (SC Cittadella-Italia) na Bevis Mugabi (Anorthosis Famagusta-Cyprus).

Mbali na Mato, wanamichezo mbalimbali waliofanya vizuri kwa mwaka 2024 walitunukiwa tuzo hizo za FUFA.