Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Suarez, Cavani waifanya kitu mbaya Russia

Muktasari:

  • Suarez alifunga bao la kwanza kwa mpira wa adhabu uliokwenda moja kwa moja wavuni kabla ya beki wa Russia Denis Cheryshev kujifunga mwenye na Edinson Cavani alipachika bao la tatu katika dakika 93.

Moscow, Russia. Washambuliaji Luis Suarez na Edinson Cavani wamekiongoza kikosi cha Oscar Tabarez  cha Uruguay kuwachapa wachezaji 10 wa Russia kwa mabao 3-0, katika mchezo wa mwisho wa Kundi A katika Kombe la Dunia.

Ushindi huo umeifanya Uruguay kuongoza Kundi A ikiwa na pointi 9, wakifuatiwa na wenyeji Russia iliyoshika nafasi ya pili huku Saudi Arabia ikiwa ya tatu na Misri ya mwisho.

Suarez alifunga bao la kwanza kwa mpira wa adhabu uliokwenda moja kwa moja wavuni kabla ya beki wa Russia Denis Cheryshev kujifunga mwenye na Edinson Cavani alipachika bao la tatu katika dakika 93.

Russia ilicheza karibu saa nzima wakiwa wachezaji 10, baada ya mchezaji wake Igor Smolnikov kupewa kadi mbili za njano na nyekundu katika kipindi cha kwanza.

Smolnikov ataikosa mechi ijayo jambo lililomfanya kocha wake Stanislav Cherchesov kupiga chupa ya maji teke kuonyesha hasira zake.