Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Straika Namungo awataka wachezaji kuchangamkia fursa nje

Muktasari:

Siri imefichuka ya wachezaji wazawa kushindwa kupambana wanapopata nafasi ya kucheza nje ya nchi kwamba wengi wao mawazo yao yapo Simba na Yanga.

MSHAMBULIAJI  wa  Namungo FC, Mburundi Bigirimana Blaise amesema licha ya wachezaji wazawa kuwa na vipaji vya hali ya juu, amebaini kinachowakwamisha kutikisa nje ya mipaka ya nchi zao.
Blaise anasema Ligi Kuu Bara ipo juu kuliko nchini kwao Burundi, ila anachoshangazwa ni namna wachezaji wazawa wanavyoshindwa kupanua akili zao juu ya maisha yao ya soka kuhakikisha wanafika mbali.
Ametolea mfano wa Shiza Kichuya ambaye alikuwa anang'ara akiwa Simba na sasa amekuwa kama hayupo kwenye mchezo baada ya kwenda kucheza nchini Misri.
Kitu alichokiona kwa wachezaji wazawa alikitaja kwamba ni waoga wa kuthubutu akidai wengi wao akili zao zipo Simba na Yanga na hata wakitakiwa na timu kubwa nje wanakosa kuona fursa.
"Nilisikitika kusikia Ibrahim Ajibu ameshindwa kukubali ofa ya TP Mazemnbe, ujue hii ni ajabu, unaona sisi tukija hapa tunavyopambana sio kwamba hatupendi nchi yetu ama familia bali tunatafuta maisha.
" Ndio maana wakija wageni wanafanikiwa zaidi halafu wanaondoka, ukiwa mchezaji wa kigeni kuna vitu lazima utajifunza na utakuwa unajituma ukijua wazi kilichokupeleka nchi ya watu  ni kazi"anasema.
Amewataka waige mfano wa wachezaji wa Kitanzania kama Mbwana Samatta, Simon Msuva, Hassan Kessy, Abdi Banda, Farid Mussa na Himid Mao ambao wanapambana nje.
"Hii itawasaidia kwenye timu yao ya taifa kuwa imara, sio wanaenda kucheza nje halafu wanawaza Simba na Yanga watakuwa hawafiki mbali hata kina Samatta, Msuva, Banda, Mao, Farid na Kessy walikuwa kama wao," anasema.