Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Stars jeshi kamili

Muktasari:

  • Stars inajifua kwa ajili ya maandalizi ya mechi za kufuzu Fainali za Mataifa Afrika (Afcon 2023).

TIMU ya Taifa Tanzania ‘Taifa Stars’ imeendelea na mazoezi katika uwanja wa Benjamin Mkapa ikijiandaa na mchezo wa kufuzu Kombe la Mataifa Afrika dhidi ya Niger.

Stars itacheza na Niger Juni 4 nchini Benin kisha itacheza na Algeria Juni 8 nchini katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Katika mazoezi hayo mastaa wote wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi wakiongozwa na Mbwana Samatta (Royal Antwerp) na yeye alikuwa uwanjani.

Wachezaji wengine ni Himid Mao (Ghazl El Mahalla), Kelvin John (KRC Genk), Novatus Dismas (Maccabi Telaviv), Ben Starkie (Spalding United), Haji Mnonga (Weymouth Fc) na Ibrahim Joshua (Tusker).

Upande wa wachezaji wanaocheza ndani ya nchi ni wachezaji wa Yanga, Abuutwalib Mshery, Dickson Job, Kibwana Shomari, Bakari Mwamnyeto, Farid Mussa, Feisal Salum na Salum Abubakari.

Upande wa Simba, Kennedy Juma, Aishi Manula, Kibu Dennis, Mohamed Hussein na Mzamiru Yassin.

Wachezaji wengine Aziz Andambwile (Mbeya City), Nickson Kibabage (KMC), George Mpole (Geita Gold) na Simon Msuva (Hana timu).