Staa Simba afumua kikosi

Muktasari:
- Kitendo hicho kimemfanya Suluja aliyewahi kutamba na Pamba ya Mwanza, kuliambia Mwanaspoti kuwa amefurahishwa na hatua hiyo inayoonyesha uwajibikaji.
NYOTA wa zamani wa Simba, Mnenge Suluja amempongeza Rais wa Heshima wa klabu hiyo, Mohamed Dewji ‘Mo’ kwa kuwawajibisha wajumbe wa bodi baada ya timu hiyo kufanya vibaya, huku akishauri kikosi kufumuliwa kikosi chote cha sasa cha timu hiyo, kisha kusukwa upya kwa ajili ya msimu ujao.
Kitendo hicho kimemfanya Suluja aliyewahi kutamba na Pamba ya Mwanza, kuliambia Mwanaspoti kuwa amefurahishwa na hatua hiyo inayoonyesha uwajibikaji.
“Wanachokifanya nakubali ndiyo inavyotakiwa MO alichofanya ni sahihi tuone hao watakaokuja watatufikisha wapi. Timu nzima inatakiwa ifanyiwe marekebisho sehemu zote zimepwaya, wafanye usajili mzuri ili kuepusha haya, watu watakaowekwa wajali maslahi ya Simba.”
Kaimu Mwenyekiti wa Simba Mkoa wa Mwanza, Salya Ludanha alisema; “Tunachokihitaji ni furaha kama kuna kiongozi ameona hajatosha aachie ngazi aje mwingine Simba ni yetu sote. Tupate sajili zitakazorudisha furaha tunachotaka ni kuona usajili unaendelea na watu kuwajibika.”