Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

SRRH yashtuka, kuanzisha Fitness Club

Muktasari:

  • Kuhamasisha jamii kufanya mazoezi kuepukana na magonjwa yasiyoambukizwa kama shinikizo la damu, kisukari, kiarusi.

Mganga Mfawidhi wa  hospitali hiyo, Dk John Luzila amesema hayo jana wakati wa maandalizi ya kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani inayofanyika leo Mei Mosi, ambapo aliweka bayana kwamba lengo ni kufanya mwendelezo wa kuboresha afya za watumishi wa SRRH.

Dk Luliza ameyasema hayo baada ya mazoezi ya viungo na kupanda miti katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinganya mkoani Shinyanga,

“Ili kuhamasisha wananchi katika kulinda afya zao kuepukana na magonjwa yasiyo ya kuambukizwa kama shinikizo la damu, kiarusi na kisukari tunafanya utaratibu wa kuanzia kituo cha mazoezi kitaitwa Shinyanga Regional Referal Hospital (SRRH) Fitness Club ” amesema Dk. Luzila.

Pia ameendelea kwa kusema kuwa, “Katika kuadhimisha wiki hii ya wafanyakazi ambayo kilele chake ni kesho hospitali imeweka huduma ya uchunguzi wa shingo ya kizazi na homa ya ini.”

Kwa upande wa Daktari wa Upasuaji wa Mifupa, Geofrey Mboye amesema wafanyakazi katika hospitali hiyo watashiriki mazoezi mara mbili kwa mwezi kuongeza mwamko kwa wafanyakazi wengine na jamii nzima,

“Watu wanalegalega kufanya mazoezi hasa kwa watumishi bado mwamko ni mdogo huwezi kumwambia mgonjwa atanye mazoezi wakati sisi wenyewe katufanyi,” amesema Dk Mboye.

Ofisa Muuguzi Msaidizi wa hospitali hiyo, Mwanzenu Mbaruku amesema anaomba viongozi waangalie kwa ndani suala zima la mishahara kwa wafanyakazi,

“Siku ya Mei Mosi ni muhimu sana kwetu tunaomba viongozi watuangalie sisi wafanyakazi kuhusiana na suala la mshahara kwa undani zaidi ni hilo,” amesema Mwanzenu.

Aidha, Ofisa Afya Mazingira, Emiliana Charles amesema takribani miti 500 imepanda siku ya leo ambayo italeta hewa safi na upatikanaji wa matunda kwa wagonjwa hospitalini hapo,

“Kupitia miti hii itasaidia wagonjwa kupata hewa safi, kivuli na upatikanaji wa matunda kwa wagonjwa,” amesema Emiliana.