Spurs ya Mourinho yaitangulia Aston Villa ya Samatta

Muktasari:

Tottenham Hotspur imefanikiwa kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-1 dhidi ya Aston Villa ya Mbwana Samatta kwenye Uwanja wa Villa Park.

London, England. Tottenham Hotspur imefanikiwa kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-1 dhidi ya Aston Villa ya Mbwana Samatta kwenye Uwanja wa Villa Park.

Wenyeji Aston Villa walioanza mchezo huo kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la kuongoza katika dakika 9, baada ya beki wa Spurs, Toby Alderweireld wakati akijaribu kuzuia krosi iliyokuwa ikielekea kwa Samatta.

Baada ya bao hilo Villa ilipoteza nafasi kadhaa za wazi kufunga kutokana na kukosa umakini kwa washambuliaji wake.

Spurs ilisawazisha bao dakika 27, kupitia beki wake aliyejifunga Alderweireld akiunganisha kwa shuti kali kona iliyoshindwa kuokolewa na wachezaji wa Villa.

Jahazi la Villa lilizidi kuzama baada ya Spurs kupata bao la pili katika 45+2, kupitia mkwaju wa penalti wa Son Heung-min ambao uliokolewa na kipa kabla ya Mkorea huyo kuwai na kumalizia mpira wavuni.

Vikosi

Aston Villa XI: Reina, Engels, Konsa, Hause, Guilbert, Drinkwater, Douglas Luiz, Targett, El Ghazi, Samatta, Grealish

Aston Villa akiba: Borja Baston, Taylor, Nakamba, Hourihane, Trezeguet, Nyland, Elmohamady

Tottenham Hotspur XI: Lloris, Aurier, Sanchez, Alderweireld, Davies, Winks, Dier, Lucas Moura, Alli, Bergwijn, Son

Tottenham akiba: Vertonghen, Lo Celso, Gazzaniga, Ndombele, Skipp, Fernandes, Tanganga. Referee: Martin Atkinson (W Yorkshire)