SportsPesa yamuibua mshindi Bajaj Kigoma

Muktasari:

Shindano hilo la Sportpesa limekuwa likiwaibua washindi kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Dar es Salaam. Kampuni ya SportPesa imeingia mkoani Kigoma, baada ya Hamisi Kanuma kushinda Bajaj ya nne katika promosheni inayoendelea ya shinda zaidi na SportPesa.

Hii ni mara ya kwanza mkoa huo kutoa mshindi wa shindano hilo baada ya Kanuma kubashiri kwa ufasaha na SportPesa na namba yake kuingia katika droo kabla ya kushinda Bajaj mpya.

Akizungumza jana, Kanuma alisema anatarajia kutumia Bajaj hiyo kupata kipato ambacho kitainua maisha yake na familia.

“Nimefurahi kushinda Bajaj kutoka SportPesa naamini itatusaidia kuinua maisha yetu, nitaindesha mwenyewe kwa kuitumia kufanya biashara,”alisema Kanuma mwenye miaka 19.

Mshindi huyo ametoa rai kwa Watanzania kushiriki mchezo wa kubahatisha kupitia SportPesa.

Hii ni mara ya kwanza kwa SportPesa kupata mshindi wa Bajaj kutoka Kigoma hatua inayothibitisha kuwa mchezo huo unachezwa na idadi kubwa ya watu kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Jumla ya Bajaj nne zimepata washindi wakitokea maeneo tofauti nchini, baada ya kubashiri kwa ufasaha mchezo wa kubahatisha kupitia SportPesa.