Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

SportsPesa yampa nyumba bondia Mwakinyo

Muktasari:

Mwakinyo alipata umaarufu hivi karibuni baada ya kumchapa Sam Eggington wa Uingereza kwa TKO ambaye kabla ya kipigo alikuwa bondia namba nane duniani kwenye uzani wa welter

Dar es Salaam. Mambo yameanza kumnyookea Bondia Hassan Mwakinyo baada ya kupata udhamini mnono Wa kampuni ya Sportpesa Tanzania wa miaka mitatu.

Mwakinyo amesaini mkataba huo leo Alhamisi mbele ya Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe.

Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Sportpesa, Abass Tarimba alisema mkataba huo utamuwezesha Mwakinyo kufikia malengo yake kimataifa.

"Ni mkataba mnono, siwezi kusema ni kiasi gani, lakini ni mkataba wenye fedha nyingi," alisema Tarimba.

Ingawa Mwakinyo ameeleza kuwa katika mkataba huo, atapewa vifaa vyote vya michezo sanjari na nyumba.

"Nimepewa nyumba na Sportpesa ambayo mimi ndiye mmiliki," alisema Mwakinyo.

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakymbe alisema ameuchungulia mkataba wa Mwakinyo kama shahidi unakwenda kumbadilishia maisha yake.

"Ni mkataba mnono, unamtoa Mwakinyo katika maisha ya zamani, kifupi anatoka kwenye mkweche," alisema Mwakyembe.