Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Singida Fountain Gate yafungiwa kusajili

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetoa taarifa ya kufungiwa kusajili wachezaji kwa klabu ya Singida Big Stars inayoshiriki Ligi Kuu baada ya Nicholas Gyan kufungua kesi ya madai dhidi ya timu hiyo.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa uamuzi huo ulikuja baada mchezaji huyo raia wa Ghana alifungua kesi FIFA akidai malipo ya ada ya usajili na malimbikizo ya mishahara

"Uamuzi huo umefanywa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu FIFA baada ya mchezaji Nicholas Gyan kushinda kesi ya madai dhidi ya kabla hiyo. Mchezaji huyo alifungua kesi FIFA akidai malipo ya ada ya usajili na malimbikizo ya mshahara”

"Klabu hiyo ilitakiwa iwe imemlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa lakini haikutekeleza hukumu hiyo” imesema taarifa hiyo