Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Singano ataja ugumu wa Mexico

SINGANO Pict

Muktasari:

  • Huu ni msimu wa tatu mfululizo kwa beki huyo wa timu ya taifa ‘Twiga Stars’ kuichezea timu hiyo akifanikiwa kuingia kwenye kikosi cha kwanza moja kwa moja mbele ya nyota kibao kutoka mataifa ya Ulaya.

BEKI wa FC Juarez inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake nchini Mexico, Julietha Singano amesema ugumu wa ligi hiyo unamfanya aonyeshe jitihada zaidi.

Huu ni msimu wa tatu mfululizo kwa beki huyo wa timu ya taifa ‘Twiga Stars’ kuichezea timu hiyo akifanikiwa kuingia kwenye kikosi cha kwanza moja kwa moja mbele ya nyota kibao kutoka mataifa ya Ulaya.

Akizungumzia kiwango chake ndani ya misimu mfululizo, Singano alisema ligi ya nchi hiyo ni ngumu hivyo ili upate nafasi basi unapaswa kujituma na kujitoa haswa.

“Ni kujituma ligi ya kule ni ngumu hivyo kila unapopata nafasi ya kucheza basi unapambana na sio rahisi kocha kukupa nafasi wewe ndani ya misimu yote hivyo ni juhudi binafsi,” alisema na kuongeza:

“Kwa sasa ligi nimeizoea lakini bado lugha changamoto kwa sababu wanaongea Kihispaniola lakini kuna lugha za mpira tunaelewana na Kiingereza wanaongea mara chache.”

Singano amekuwa mchezaji muhimu kikosini hapo tangu ajiunge nao mwaka 2022 akitokea Simba ambako aliwapa ubingwa mara mfululizo.

Licha ya kuisaidia timu pia amekuwa nyota anayetajwa kuingia kwenye kikosi bora cha kila mwezi nchini humo akishindanishwa na nyota wakubwa wanaotoka nchi nyingine.