Simba yatinga Boko Veterans na gari la Al Ahly

Muktasari:

Simba wataikabili Yanga ikitambia nyota wao Meddie Kagere na Emmanuel Okwi waliopo kwenye orodha ya wakali wa mabao katika Ligi Kuu Bara, lakini watani zao wakijivunia Ibrahim Ajibu anayetisha kwa kuasisti mabao na Heritier Makambo anayeongoza kwa mabao.

Kikosi cha Simba kinaendelea na mazoezi yake jioni ya leo Ijumaa kwenye Uwanja wa Boko Veterans kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wake wa Ligi Kuu dhidi ya Yanga kesho Jumamosi.

Simba imetua uwanjani hapo na basi ambalo lilitumiwa na  Al Ahly.

Kikosi cha Simba kilifika katika uwanja wa Boko Veterans saa 09:40 kwa ajili ya mazoezi. Basi ambalo walikuja nalo uwanjani hapa Simba no lile ambalo walilitumia Al Ahly.

Tangu Al Ahly wanafika mpaka kuondoka walitumia basi hilo ambalo linaitwa Higer. Simba watafanya mazoezi ya mwisho. Ikumbukwe mechi ya mzunguko wa kwanza Simba walitoka suluhu ya bila kufungana na Yanga.

Simba na Yanga zinakutana kwenye pambano lao la 102 tangu aanze kukutana katika ligi iliyoasisiwa mwaka 1965, huku Yanga wakiwatambia wenzao kwa kushinda mechi 36 dhidi ya 30 za wenzao wa Msimbazi, lakini mechi 35 zikimalizika bila kupata mbabe.

Simba wataikabili Yanga ikitambia nyota wao Meddie Kagere na Emmanuel Okwi waliopo kwenye orodha ya wakali wa mabao katika Ligi Kuu Bara, lakini watani zao wakijivunia Ibrahim Ajibu anayetisha kwa kuasisti mabao na Heritier Makambo anayeongoza kwa mabao.

Klabu hizo kongwe zinatarajiwa kuvaana wikiendi hii katika pambano lao la pili katika msimu wa 2018-2019, ikiwa ni zaidi ya minne tangu walipokutana kwenye mchezo wa mwisho uliopigwa Septemba 30 mwaka jana na matokeo kuwa suluhu.