Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yashusha winga Mmalawi

KIKOSI cha Simba kimemtambulisha Duncan Nyoni "Monster" kutoka klabu ya Silver Strikers ya nchini Malawi kwa ajili ya msimu ujao wa 2021/22.

Usajili huo ni mwendelezo wa maingizo mapya ya kikosi hicho kuelekea msimu ujao wa Ligi kuu Tanzania Bara, Kombe la Azam Shirikisho, Mapinduzi na Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF).

Winga huyo anaungana na nyota wengine waliosajiliwa katika kikosi hicho akiwemo Peter Banda aliyetokea Big Bullets ya Malawi na Yusuph Mhilu aliyetokea Kagera Sugar.

Simba inaendelea kujiimarisha baada ya kuondokewa na wachezaji wake muhimu wa kikosi cha kwanza wakiwemo Luis Miquissone aliyetimkia Al Ahly na kiungo Mzambia Clatous Chama aliyejiunga na RS Berkane ya nchini Morocco.