Simba yarejea mzigoni

KLABU ya Simba imerejea mazoezini leo asubuhi wakijiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Al Ahly utakaopigwa nchini Misri, Aprili 9.

Kikosi hicho kinachonolewa na kocha Didier Gomes kimerejea kambini baada ya mapumziko mafupi ya Sikukuu Pasaka.

Gomes alianza kwa kuwapa mazoezi mepesi wachezajj wake ili kurejea katika hali yake yao ya kawaida.

Baada ya hapo aliwapa mazoezi ya kupita katika koni huku wakichezea mpira, baada ya hapo aliwapa zoezi la kuchezea mpira.

Wakati wote wa mazoezi wachezaji hao walionekana kuwa na morali ya juu na utani wa hapa na pale.