Simba, Yanga yaahirishwa, mashabiki wadai chao

Saturday May 08 2021
kuahirishwa pic
By Clezencia Tryphone

RUDISHENI pesa zetu, ndizo kauli za mashabiki baada ya kutangazwa kuahirishwa kwa mchezo wa Simba dhidi ya Yanga leo Mei 8, 2021.
Mchezo wa Simba dhidi ya Yanga ulipangwa kupigwa leo saa 11:00 jioni na baadae kusogezwa mpaka saa 1:00 usiku kitendo ambacho Yanga walikigomea.
Mashabiki wa Yanga na Simba wameonekana kukasilishwa na sintofahamu hiyo baada ya kutolewa tangazo la kuhairishwa kwa mchezo walianza kulalama kutaka kurudishiwa pesa zao.
John Michael ambaye ni shabiki wa Simba alisema "Hii ni aibu kuanzia kwa TFF mpaka Wizara yenyewe ambayo imewafanya watangaze hii sio kabisa sasa tunataka pesa zetu," .
Huku Baraka Juma alisema "Tunadai pesa zetu na tunaenda kukaa pale ndani getini kuhakikisha tunapewa chetu ndio tuondoke,"
Amesema hii ni aibu kwa Tanzania na imeingia katika historia mbaya kwa Shirikisho hilo.

Advertisement