Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba, Yanga mtegoni CAF

Muktasari:

  • Timu 15 zimetinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu ambazo ni Etoile du Sahel, Esperance, Wydad Casablanca, Al Ahly, Pyramids, Al Hilal, Simba, Yanga, Mamelodi Sundowns, Petro Atletico, Medeama, FC Nouadhibou, TP Mazembe, Jwaneng Galaxy na Asec Mimosas.

KITENDO cha Simba na Yanga kuwekwa katika vyungu tofauti katika zoezi la upangaji wa makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu litakalofanyika Johannesburg, Afrika Kusini, Ijumaa, Oktoba 6 kinatengeneza uwezekano mkubwa wa wawakilishi hao wa Tanzania kukutana katika hatua hiyo msimu huu.

Yanga imefuzu hatua ya makundi baada ya kuitupa nje Al Merrikh ya Sudan wakati Simba imetinga baada ya kuiondoa Power Dynamos ya Zambia.

Katika droo hiyo, Simba itakuwa katika chungu cha pili pamoja na timu za CR Belouizdad, Pyramids na Petro Atletico.

Yanga yenyewe itakuwa chungu cha tatu na timu za TP Mazembe, Al Hilal na Asec Mimosas.

Kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo, kila kundi litaundwa na timu moja kutoka kila chungu kati ya vinne  ambavyo vitakuwepo katika uchezeshaji wa droo na hakuna zuio kwa timu za nchi mmoja kukutana.

"Chama cha mpira hakiwezi kuwa na timu zaidi ya mbili kutoka nchini mwake kwenye hatua ya makundi," inafafanua kanuni ya 3 ibara ya 17 ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Haitokuwa jambo la kushangaza ikiwa Yanga na Simba zitakutana katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwani imeshawahi kutokea mara nyingi nyuma kwa timu za nchi moja kukutana katika hatua hiyo.

Tangu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ianzishwe rasmi mwaka 1998, misimu 10 tofauti imeshuhudiwa timu za nchi moja kukutana katika hatua ya makundi.

Sudan na Misri ndio zinashikilia rekodi ya nchi ambazo klabu zake zimekutana mara nyingi zaidi katika hatua ya makundi ambapo kwa Sudan timu za Al Hilal na Al Merrikh zimekutana mara tatu ikiwa ni msimu wa 2021/2022, 2017 na 2009, kama ilivyo kwa Misri katika msimu wa 2012, 2010 na 2008.

Mara mbili tofauti, timu za Tunisia zilikutana katika hatua ya makundi kama ilivyo kwa Algeria wakati DR Congo na Angola timu zake zimewahi kukutana mara moja kwa kila nchi.

Kocha wa Simba, Roberto Oliveira 'Robertinho' alisema kuwa wanahitajika kuimarika zaidi katika hatua ya makundi ili wafanye vizuri.

"Jambo la muhimu kwa sasa ni kwamba tumeingia hatua ya makundi. Ni hatua ngumu ambayo tunakwenda kukutana na timu bora na imara, hivyo tunapaswa kufanyia kazi yale tuliyoonyesha mapungufu ili tuweze kufika hatua za juu zaidi.

"Katika hatua ya makundi hakuna timu nyepesi na ni lazima tufanye kazi ya ziada ili tuweze kupata kile tunachokitegemea. Nina imani na wachezaji wangu na naamini tutafanikiwa katika hilo," alisema Robertinho.

Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi alisema ndoto zake ni kuona timu yake inafanya vizuri zaidi katika mashindano hayo na anatamani maboresho zaidi ya kikosi chake.

"Tunakwenda kushindana katika hatua ya makundi. Kama tunataka kushindana kwa nguvu tunahitaji kusajili lakini sijui kama inawezekana kwa klabu. Kama kocha, muda wote unahitaji zaidi. Inawezekana, tunahitaji maboresho kidogo ili tuweze kushindana dhidi ya timu kubwa," alisema Gamondi.