Simba, Yanga kukipiga Desemba 11

Friday September 10 2021
derby pic
By Mwandishi Wetu

Ratiba ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2021/22 imetangazwa leo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu, Almas Kasongo na mechi ya watani wa jadi ikipigwa Desemba 11.

Simba na Yanga zitafungua Ligi kwa mechi ya ngao ya jamii itakayopigwa Septemba 25 kabla ya Ligi kuanza 27.

Msimu uliopita Yanga alianza kwa sare mechi ya kwanza na kushinda mechi ya pili ambayo Simba walikuwa wenyeji.

Advertisement