Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yalala Ethiopia, kutua Kinshasa leo

WAWAKILISHI pekee wa Afrika Mashariki kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, jana usiku walilala Jijini Adis Ababa Ethiopia na leo watatua Kinshasa, DR Congo.

Simba iliondoka Dar es Salaam jana saa 10 jioni kupitia Ethiopia ambapo walitua Addis saa 1 usiku na leo saa 4:25 wataondoka na kutua Kinshasa saa 6:10 mchana.

Kumbuka Mwanaspoti ambalo linatimiza miaka 20 Ijumaa hii, ndilo gazeti pekee la Tanzania litakalokuwa linakuripotia laivu kila hatua itakapokanyaga Simba.

Simba imepania kufanya maajabu kwenye mchezo huo na kuanza kwa kasi ya aina yake kwenye hatua hiyo muhimu. Kumbuka msimu uliopita Simba iliwapiga AS Vita kwenye Uwanja wa Mkapa na kuwanyima tiketi ya kutinga robo fainali ya ligi hiyo yenye heshima zaidi Afrika.

Tangu wanaondoka Dar es Salaam jana wachezaji wa Simba wameonekana kuwa wenye mzuka wa aina yake jambo ambalo linatia matumaini kwa wawakilishi hao wa nchi.